Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yachaguliwa kuwa kituo cha mafunzo cha magonjwa ya moyo katika mfumo wa umeme wa moyo kwa wataalamu wa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imechaguliwa kuwa kituo cha mafunzo cha magonjwa ya moyo katika mfumo wa umeme wa moyo kwa wataalamu wa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa kwa njia ya mtandao na wataalamu wa magonjwa ya moyo na matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo kutoka Hospitali ya Shifa iliyopo nchini Misri. Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa magonjwa ya moyo Dkt. Tatizo Waane alisema mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa wakati wa kambi maalum za matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo zitakazokuwa zinafanyika katika Taasisi hiyo. Dkt. Waane ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mzibuaji wa mishipa ya damu ya moyo alisema katika kambi hizo maalum za matibabu licha ya kutibu, wataalamu wanabadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa wenye tatizo hilo la moyo unaokwenda kwa haraka. “Katika kambi hizi huwa mafunzo ya...