Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Mitambo mipya ya Kisasa ya Matibabu ya Moyo ya Cathlab na Carto 3 System katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kuzindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) mara alipotembelea chumba cha Wodi ya Watoto wenye uhitaji wa Uangalizi maalum kabla ya kuzindua mitambo ya Catheterization Laboratory pamoja na Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system katika Taasisi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) Profesa Mohamed Janabi alipokuwa akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa mitambo hiyo ya Kisasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi wakati akitoka kutembelea Wodi ya Watoto katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo pamoja na kukagua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete pamoja na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo. 

Picha na Ikulu

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)