Posts

Showing posts with the label Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Shinyanga waitwa kupima moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga alipomtembelea ofisini kwake leo kabla ya kuanza kwa kambi maalumu ya siku tano ya  Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanyika katika  Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga (SRRH). Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mwananchi aliyefika  katika  Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga (SRRH) kwaajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga (SRRH) Dkt. Luzila Boshi akifuatiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RMO) Dkt. Yudas Ndungile. ***************************************************************************************************************************** Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ali...

Rais Dkt. Samia aipongeza JKCI kwa kuwafuata wananchi mahali walipo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Taasisi, Mashirika ya Umma   na Kampuni ambazo Serikali ina hisa wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango iliyofanyika jana Ikulu   jijini Dar es Salaam. ***********************************************************************************************************************************************************************************  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kutoa huduma ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa kuwafuata wananchi mahali walipo. Pongezi hizo amezitoa jana wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi, Mashirika ya Umma   na Kampuni ambazo Serikali ina hisa iliyofanyika Ikulu   jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Dkt. Samia alisema taasisi ambazo zinatoa huduma ya kuisaidia jamii kama ambavyo JKCI inafanya zinatakiwa...

Pinda: Kupatikana kwa matibabu ya kibingwa ya moyo nchini kumeokoa maisha ya watu wengi

Image
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisoma folder lenye taarifa za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za upimaji wa moyo zinazotolewa katika zoezi la kupima magonjwa hayo     linalofanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Galiyaya akimpima kiwango cha sukari kwenye damu Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Ole Shangai aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma. Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima uwiano baina ya urefu na uzito Mbunge wa Momba Mhe. Condester Sichalwe aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa ...