Wafanyakazi JKCI Dar Group wapewa onyo dhidi ya ubadhilifu wa mali za Umma
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali hiyo hiyo jana jijini Dar es Salam wakati wa hafla ya kuwatambua wafanyakazi bora kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi duniani. Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuwatambua wafanyakazi bora kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani. Na JKCI **************************************************************************************************** Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group wametakiwa kuepuka ubadhilifu katika matumizi ya mali za umma ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya vifaa vya ofisi pamoja na vitendo vya uhujumu uchumi vinavyoweza kuathiri utendaji wa kazi za taasisi. Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa JKCI Hospital...