Huduma za Moyo zawafikia wananchi Njombe, DC atoa ombi Maalumu
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Juma Sweda akimsikiliza daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ili kuona huduma za matibabu zinazotolewa.
Daktari wa kinywa na meno wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Hospitali ya Dar Group Joachim Mvungi akichunguza kinywa cha mwananchi
aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa afya wakati wa maonesho ya Usalama na Afya
Mahali pa Kazi yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema
Mkoani Njombe.
Afisa Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rajabu
Hamis akiwaelezea wakazi wa Njombe huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo
walipotembelea banda la JKCI lililopo katika maonesho ya Usalama na Afya Mahali
pa Kazi yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema Mkoani
Njombe.
Na JKCI
*********************************************************************************************
Wataalamu
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group wameombwa
kuendelea kufika katika Mkoa wa Njombe kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya
moyo kutokana na ongezeko la uhitaji wa huduma hizo mkoani humo.
Ombi hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Juma
Sweda, alipotembelea banda la JKCI katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa
Kazi yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema ili kujionea
huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa mbalimbali zinazotolewa katika banda
hilo.
Mhe. Sweda alisema wananchi wa Njombe wamekuwa wakisafiri umbali
mrefu kufuata huduma za moyo hivyo basi
uwepo wa wataalamu hao kupitia maonesho hayo umeleta nafuu kubwa na
kuongeza uelewa kuhusu magonjwa ya moyo na yasiyoambukiza.
“Wakazi wa Njombe msisite kutumia fursa hii kufanya uchunguzi wa
magonjwa ya moyo na kupata elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwani
yamekuwa tishio kubwa katika jamii yetu”,
alisema Mhe. Sweda.
“Tunawashukuru sana
wataalamu wa JKCI kwa kufikisha huduma hizi adhimu katika mkoa wetu. Tunaomba
baada ya maonesho haya mpange tena kufika Njombe kutoa huduma zaidi ili kuwafikia wananchi wengi wenye uhitaji wa
huduma hizo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi
waliopata huduma katika banda la JKCI waliishukuru serikali kwa kuruhusu
kufanyika kwa maonesho hayo ambayo yamewapa fursa ya kuchunguza afya zao bila
malipo karibu na maeneo yao.
Emanuel Elius, mkazi wa Njombe alisema
amefaidika na huduma za uchunguzi wa moyo aliyoipa kwani hiyo ni mara yake ya
kwanza kufanya vipimo vya moyo na kupata
elimu muhimu kuhusu afya yake.
“Nilikuwa nikitumia sigara kwa muda wa miaka
sita lakini leo nimepima moyo na kushauriwa kuacha uvutaji wa sigara ili kujikinga na matatizo ya moyo
ikiwemo kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo”, alisema Emanuel.
Naye Rose Mvile mkazi wa
Njombe alisema ameridhishwa na huduma alizopata, kutokana na ukarimu wa
wataalamu wa JKCIna amepata fursa ya
kuhudumiwa na madaktari bingwa bila gharama yoyote ile.
“Wanawake tuna majukumu mengi katika familia hivyo
tunapaswa kutumia fursa hizi kuchunguza afya zetu mapema ili kulinda familia
zetu pia ukifika katika banda la JKCI utapata elimu ya lishe bora ambayo
itakusaidia kufahamu ”, alisema Rose.
Huduma za
upimaji zinazotolewa katika kambi ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
mkoani Njombe ni pamoja na uchunguzi wa magonjwa ya moyo, kipimo cha shinikizo
la damu (presha), kipimo cha sukari kwenye damu, kipimo cha mafuta mwilini,
uwiano baina ya uzito na urefu (BMI), vipimo vya mfumo wa umeme wa moyo na
jinsi moyo unavyofanya kazi na elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Comments
Post a Comment