Posts

Showing posts with the label JKCI

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu  ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu ya moyo mara baada ya kuisaini jana jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pe...

JKCI kuwa kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto Afrika Mashariki na Kati

Image
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Che Mingjian, wakibadilishana  Mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete eneo la Mloganzila kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto Afrika Mashariki na Katipamoja na mradi wa ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu, hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Che Mingjian, wakitia saini Mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete enelo la Mloganzila kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto  Afrika Mashariki na Kati  pamoja na mradi wa ushirikiano wa kiuchumi n...

JKCI na Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la Italia wasaini mkataba wa kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo Afrika

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge  na Rais wa Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la nchini Italia Palumbo Vincenzo wakibadilishana mkataba wa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo  barani Afrika wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Rais wa Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la nchini Italia Palumbo Vincenzo wakionesha mkataba wa kuwatibu watoto wenye matatizo  ya moyo waliopo barani Afrika wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. ************************************************************************************************************************************************************************************************************************* Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)...

GSM Foundation na Yanga wachangia milioni 50 za matibabu ya moyo kwa watoto

Image
Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 fedha zilizotolewa na GSM Foundation na klabu hiyo kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea taasisi hiyo leo kwa ajili ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 50 fedha zilizotolewa  na GSM Foundation na klabu hiyo kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said alipotembelea taasisi hiyo leo kwa ajili ya kukabidhi hundi ya shilingi...

Zanzibar waendelea kupata huduma za matibabu ya moyo

Image
Wakazi wa Zanzibar wakiwa katika foleni ya kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport. Wakazi wa Zanzibar wakipata huduma mbalimbali katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akiwafundisha wanafunzi namna huduma za matibabu ya moyo zinavyofanyika wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport. Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Heart Team Africa Foundation (HTAF) Linda Gideon akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Zanzibar mara baada ya kuchangia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kwa kununua T-shirt wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika v...

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo ya kumshukuru Mke wa Rais wa Msumbiji Mhe.   Mama Gueta Selemane Chapo kwa kutembelea taasisi hiyo na kuahidi kushirikiana nayo katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi   Mke wa Rais wa Msumbiji Mhe. Mama Gueta Selemane Chapo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam   kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Mke wa Rais wa Msumbiji Mhe. Mama Gueta Selemane Chapo akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolew...

Watu 383 wachunguzwa moyo Singida

Image
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga akimsikiliza daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago alipotembelea banda la taasisi hiyo  kuangalia huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yaliyofanyika   katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida. Wananchi wa Singida wakisubiri kupata huduma za  uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yaliyomalizika jana  katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.  ******************************************************************************************************************************************************************************************* Na Jeremiah Ombelo - Singida...

JKCI yatumia akili mnemba na teknolojia za kidijitali katika matibabu ya moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago akizungumza na mkazi wa Singida aliyefika katika banda la taasisi hiyo  kupata  huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yaliyofanyika    katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida . ******************************************************************************************************************************************************************************************************************  Na Jeremia Ombelo - Singida  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elias ...

Viongozi watembelea banda la JKCI maonesho ya Osha

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) na kiwango cha oksijeni mwilini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus aliyetembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida. Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuangalia huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wanazozitoa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Dkt. Edith Rwiza akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika maonesho ...

Banda la JKCI lawavutia wananchi kupima moyo

Image
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la JKCI kwaajili ya kuangalia huduma wanazozitoa katika  maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) mkazi wa Singida aliyefika katika viwanja vya maonesho Mandewa kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa bila malipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi. Mkurugenzi wa Usalama na Afya kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Jerome Materu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika k...

Singida wafurahia huduma za matibabu ya moyo

Image
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mkazi wa Singida aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa bila malipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya maonesho Mandewa mkoani Singida Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Devotha Bertram akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mkazi wa Singida aliyefika katika Maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yanayofanyika katika viwanja vya maonesho Mandewa mkoani Singida. Na: Jeremiah Ombelo ************************************************************************************************************* Wananchi wa Mkoa wa Singida wamepongeza huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) k...