Banda la JKCI lawavutia wananchi kupima moyo
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira
na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la JKCI kwaajili ya
kuangalia huduma wanazozitoa katika
maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi
yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) mkazi wa
Singida aliyefika katika viwanja vya maonesho Mandewa kwaajili ya kupata huduma
za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa bila malipo katika Maonesho ya
Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi.
Mkurugenzi wa Usalama na Afya kutoka Wakala wa Usalama na
Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Jerome Materu akisaini kitabu cha wageni
alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho
ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika
viwanja vya Mandewa mkoani Singida.
Mkazi wa Singida akipewa ushauri wa kiafya kuhusiana na magonjwa ya moyo kutoka kwa daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elias Birago wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya maonesho Mandewa mkoani Singida.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima kiwango cha sukari kwenye damu
mtoto aliyefika na wazazi wake katika banda la JKCI kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu
ya moyo zinazotolewa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya
Mahali Pa kazi yanayofanyika mkoani Singida.
Comments
Post a Comment