Uwekezaji sekta ya afya wawezesha utalii tiba nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wataalamu wa afya walioshiriki kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika nchini Comoro mwaka 2024 wakati wa kupokea ripoti ya kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akipokea ripoti ya kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika nchini Comoro mwaka 2024 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kupitia na kupokea ripoti hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisiya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akiwasilisha taarifa ya ripoti ya kambi maalumu ya matibabu
iliyofanyika nchini Comoro kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe
wakati wa hafla fupi ya kuwasilisha ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kambi
hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya
Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)
Mkurugenzi Mtendaji Hospitaili ya Benjamini Mkapa Prof. Abel
Makubi akichangia wakati wa kuwasilisha ripoti ya kambi maalumu ya matibabu
iliyofanyika nchini Comoro kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe
leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya
Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya
Benjamin Mkapa (BMH).
Mkurugenzi Mtendaji waTaasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya akichangia wakati wa kuwasilisha ripoti ya kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika nchini Comoro kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya Global link Abdulmalik Molel
akifafanua jambo wakati wa kuwasilisha ripoti ya kambi maalumu ya matibabu
iliyofanyika nchini Comoro kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe
leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya
Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya
Benjamin Mkapa (BMH)
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuwasilisha ripoti ya kambi maalumu ya
matibabu iliyofanyika nchini Comoro kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif
Shekalaghe leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),
Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)
Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya ikiwemo kununuliwa kwa vifaa tiba vya kisasa na kusomesha wataalamu kumewezesha kutolewa kwa huduma ya utalii tiba hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe wakati akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kupokea taarifa ya awali ya kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika
mwishoni mwa mwaka jana nchini Comoro.
Dkt. Shekalaghe alisema wagonjwa wengi wanatoka katika nchi
zao na kwenda kutibiwa katika nchi
zingine kwaajili ya kufuata utaalamu na vifaa tiba vya kisasa vilivyoko huko vitu
ambavyo vinapatikana hapa nchini.
“Kazi ya upimaji iliyofanyika ni kubwa na imeiheshimisha nchi
yetu, tumeweza kuokoa maisha ya wenzetu waliokuwa wanachangamoto mbalimbali za
kiafya pia tumeimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati yetu na Comoro kwani
Tanzania na Comoro tuna uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo ya afya”.
“Ninamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kuimarisha sekta ya afya kwani ametoa fedha nyingi ambazo zimenunua vifaa tiba
vya kutosha na vya kisasa pia amewasomesha wataalamu wengi katika ngazi ya ubingwa
bobezi”, alisema Dkt. Shekalaghe.
Dkt. Shekalaghe alisema katika kambi hiyo madaktari bingwa
kutoka hospitali ya Taifa na maalumu
walikwenda katika hospitali ya Taifa ya EL Maarouf kutoa huduma mbalimbali za
matibabu na uchunguzi kwa wananchi wa Comoro.
“Ninawapongeza kwa huduma mliyoitoa nchini Comoro ninawaomba muangalie namna ambavyo mtakwenda katika nchi zingine zinazotuzunguka kama vile
Zambia na Congo kufanya kambi za matibabu kama walivyofanya Comoro.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge ambaye alikuwa mratibu wa kambi hiyo alisema
walikwenda nchini Comoro kuimarisha utalii tiba na kuendeleza mahusiano yaliyokuwepo baina ya
nchi hizo mbili.
Dkt. Kisenge alisema
katika kambi hiyo ya matibabu ya siku tano waliona watu 2779 hii ikiwa na sawa
na kuona watu 550 kwa siku ambapo wataalamu kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na
Ubongo Muhimbili (MOI), JKCI, Hospitali ya Taifa Muhimbi (MNH), Taasisi ya
Saratani Ocean Road na Hospitali ya Benjamini Mkapa walitoa huduma za kibingwa
bobezi za magonjwa mbalimbali kwa wananchi.
“Tunashukuru tumeokoa maisha ya wenzetu kati ya watu
tulliowaona 226 walipewa rufaa ya kuja kutibiwa katika hospitali zetu ambapo
hadi sasa ni asilimia 30 wameshakuja hapa nchini kutibiwa na kwa upande wa JKCI
kuna ambao tumewatibu na kuwawekea vifaa visaidizi vya moyo ikiwemo betri za
moyo “Pace maker”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge alisema katika kambi hiyo walibadilishana ujuzi wa kazi na wataalamu wa afya wa Comoro, wametangaza
fursa za biashara zilizopo na wametangaza huduma ya utalii tiba inayopatikana
hapa nchini kwani wananchi wengi wa Comoro wanatibiwa Ufaransa hivyo
waliwaeleza fursa za matibabu zinazopatikana hapa nchini.
“Nimeona hizi hospitali zetu kubwa zikishirikiana kwa pamoja
tunaweza kutoa huduma kubwa ya matibabu kwa watu wengi kwa wakati mmoja
ninashukuru kwa ushirikiano tulioufanya tukiwa nchini Comoro ninaomba ushirikiano huu uwe endelevu”,
alishukuru Dkt. Kisenge.
Katibu wa kamati ya Utalii Tiba Abdumalik Mollel ambaye
alikuwa msimamizi wa kambi hiyo ya matibabu alisema hapa nchini kuna fursa nyingi
za utalii tiba jambo la muhimu ni kuzitangaza huduma za kibingwa za matibabu zinazotolewa nje ya nchi
ili watu wengi wazifahamu.
“Baada ya kufanyika kwa kambi hii wataalamu kutoka Wizara ya
Afya Comoro watakuja nchini kutembelea hospitali zetu na
kuona miundombinu, vifaa tiba vya kisasa vilivyopo na huduma tunazozitoa kitu
ambacho kitawafanya walete wagonjwa wengi kuja kutibiwa nchini”, alisema
Mollel.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na
Ubongo Muhimbili (MOI) Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya aliwapongeza wataalamu hao waliokwenda nchini Comoro
kutoa huduma ya matibabu na kuiomba Wizara ya Afya kuangalia namna ambavyo watashirikiana na sekta binafsi
katika kuimarisha utalii tiba nchini.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) Prof. Abel Makubi alisema utalii tiba ni fursa kubwa kwa nchi ya kuinua uchumi jambo la muhimu ni kuweka mfumo wezeshi ambao utarahisisha utoaji wa huduma hiyo katika sekta za umma na sekta binafsi.
Comments
Post a Comment