Pinda: Kupatikana kwa matibabu ya kibingwa ya moyo nchini kumeokoa maisha ya watu wengi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisoma folder lenye taarifa za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za upimaji wa moyo zinazotolewa katika zoezi la kupima magonjwa hayo linalofanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Galiyaya akimpima kiwango cha sukari kwenye damu Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Ole Shangai aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma. Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima uwiano baina ya urefu na uzito Mbunge wa Momba Mhe. Condester Sichalwe aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa ...