Afisa Takwimu wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuelezea Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kibaha Nyanjige Shimote kuhusu huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto alipotembelea Shule ya Sekondari ya Bundikani iliyopo Manispaa ya Kibaha wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika Wilaya ya Kibaha.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Stella Mongela akimpima mapigo ya moyo kupitia kwenye mkono Mwanafunzi wa shule
ya Sekondari Bundikani iliyopo Manispaa ya Kibaha wakati wa kambi maalumu ya
siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba katika
kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika Wilaya ya Kibaha mkoani
Pwani.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prisca
Kiyuka akimpatia ushauri kuhusu magonjwa ya moyo mwanafunzi wa Shule ya
Sekondari Bundikani iliyopo Manispaa ya
Kibaha wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo
ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan tiba mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika
Wilaya ya Kibaha.
Daktari bingwa wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Theophil Ludovic akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bundikani
iliyopo Manispaa ya Kibaha namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo wakati wa
kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo
kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba
mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika Wilaya ya
Kibaha.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bundikani iliyopo Manispaa ya
Kibaha wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi
maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanywa
na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wilayani Kibaha.
Picha na JKCI
************************************************************************************************
Comments
Post a Comment