Dkt. Kisenge kuongoza wataalamu kambi ya matibabu ya moyo Shinyanga
Wataalamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga (SRRH) watatoa huduma za tiba mkoba
zinazojulikana kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa
kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa
Shinyanga na mikoa ya jirani.
Upimaji huu
utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 18-22/08/2025 saa 2:00 asubuhi hadi
saa 10:00 jioni katika Hospitali
ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga (SRRH) iliyopo
Mwawaza Shinganya mjini.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa
elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia
kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na
yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika
kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo
hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya
zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa
atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa
zaidi wasiliana kwa simu namba 0756568291 Dr. Luzila John Mganga Mfawidhi na 0688665508 George Mganga Afisa Habari.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”
Comments
Post a Comment