Tanzania mshindi wa pili maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara Zambia
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara ya Zambia yaliyomalizika jana jijini Lusaka. Katika maonesho hayo Tanzania ilishika nafasi ya pili katika kundi la washiriki ya kimataifa kati ya nchi 25 zilizoshiriki.
Cheti ya Tanzania kushika nafasi ya pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki katika maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara ya Zambia yaliyomalizika jana jijini Lusaka.
Zawadi ya Tanzania kushika nafasi ya pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki katika maonesho ya 97 ya Kilimo na Biashara ya Zambia yaliyomalizika jana jijini Lusaka.
*********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Tanzania imeibuka
mshindi wa pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki katika maonesho ya 97 ya Kilimo
na Biashara ya Zambia yaliyomalizika jana jijini Lusaka.
Tanzania imeshika nafasi hiyo katika
kundi la washiriki wa kimataifa ambapo mshindi wa kwanza ni Zimbabwe.
Akizungumza mara baada ya
kupokea cheti cha ushindi Balozi wa
Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule alishukuru
kwa ushindi huo na kuahidi kuendelea kutangaza huduma mbalimbali zinazopatikana
nchini kwa kila maonesho watakayoshiriki.
Mhe. Balozi Luteni Generali Mathew Edward Mkingule alisema ushindi huo ni
matunda ya kazi kubwa iliyofanya na ubalozi wa Tanzania nchini Zambia pamoja na
Taasisi zilizoshiriki maonesho hayo ambazo kwa pamoja zimepeperusha vyema
bendera ya Tanzania.
“Katika banda la Tanzania tulikuwa
tunatangaza huduma za matibabu ya kibingwa, huduma za usafirishaji na bidhaa
mbalimbali zinazopatikana nchini zikiwemo kahawa, majani ya chai, korosho, juisi,
pombe na vinginevyo. Pia tumetoa elimu na ushauri wa magonjwa mbalimbali”.
“Ni heshima kubwa kwa nchi yetu
kupata cheti cha ushindi wa pili ambacho ni ishara ya ushirikiano madhubuti
uliopo baina ya nchi zetu mbili za Tanzania na Zambia pia ni kutambua kazi
kubwa na nzuri iliyofanywa na Taasisi zetu ambazo zimeshiriki katika maonesho
haya”, alisema Mhe. Balozi Luteni
Generali Mathew Edward Mkingule.
Mhe. Balozi Luteni Generali Mathew Edward Mkingule Serikali ya Tanzania
imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya na ndiyo maana wananchi wengi wa
Zambia na nchi jirani walifika katika banda hilo kwa ajili ya kufahamu huduma
za matibabu ya kibingwa zinazopatikana nchini na kuona namna ambavyo watazipata
huduma hizo.
Taasisi zilizoshiriki katika
maonesho hayo na kutoa huduma a afya na usafirishaji katika banda la Tanzania ni
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo
Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya
Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL).
Comments
Post a Comment