Wagonjwa 12,180 kutoka nje ya nchi watibiwa Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalage akizungumza
wakati wa mdahalo wa wazi wa kitaalamu kuhusu utalii tiba nchini ulioandaliwa
na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kuadhimisha miaka kumi tangu
kuanzishwa kwake leo katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamini Mkapa Prof. Abel
Makubi akimsikiliza mtaalamu kutoka Kampuni ya Sakaar Healthtech Limited Alfred
Moshi akimuelezea kuhusu kifaa maalumu kijulikanacho kwa jina la Dozee
kinachotumika kufuatilia maendeleo ya mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani wakati
wa mdahalo wa wazi wa kitaalamu kuhusu utalii tiba nchini ulioandaliwa na Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa
kwake leo katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Dkt. Delilah Kimambo akichangia mada wakati wa mdahalo wa wazi wa kitaalamu
kuhusu utalii tiba nchini ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake leo katika Ukumbi wa
Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Wadau wa Sekta ya Afya wakisikiliza wakati wa mdahalo wa wazi
wa kitaalamu kuhusu utalii tiba nchini ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake leo katika
Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalage Akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanafunzi wa Shule za Sekondari wakati wa mdahalo wa wazi wa kitaalamu kuhusu utalii tiba nchini ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake leo katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Na: JKCI
*****************************************************************************************************
Wagonjwa 12,180 kutoka nje ya nchi wametibiwa nchini kati ya
mwaka 2021 hadi 2025 na kuongeza fursa za utalii tiba nchini.
Akizungumza wakati wa Mdahalo wa wazi wa kitaalamu kuhusu utalii
tiba nchini Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe alisema ongezeko la
wagonjwa hao kutoka 5,700 hadi kufikia 12,180 kwa kipindi cha miaka mitano
limetokana na mipango mikakati ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali.
Dkt. Shekalaghe alisema lengo la uwekezaji wa utalii tiba
nchini ni kutaka kufikia uchumi wa kati
na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha tiba utalii Afrika.
"Wizara ya Afya imeandaa muongozo wa tiba utalii nchini
unaoainisha mambo muhimu ya kuzingatia na itaendelea kutoa ufadhili wa masomo
kwa wataalamu kuputia Samia Scholarship hivyo tunategemea wataalamu kutoka
katika Taasisi zinazotoa huduma bingwa bobezi kama ya moyo watakuwepo",
alisema Dkt. Shekalaghe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Diplomasia kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje Mhe. Balozi John Ulanga alisema kumekuwa na ongezeko la utalii
tiba kwa asilimia 19 ambao imeongeza
pato la taifa kufikia Shilingi Bilioni 166.5 .
Mhe. Balozi Ulanga alisema Tanzania inapokea wagonjwa kutoka
katika nchi 16 za Afrika zikiwemo
Comoro, Burundi, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda na nyinginezo.
"Kuanzia 2021 hadi 2025 kumekuwa na ukuaji mkubwa wa
huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hHospitali ya Benjamini
Mkapa (BMH) na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road”, alisema Mhe. Balozi Ulanga
Mhe. Balozi Ulanga alisema ifikapo mwaka 2030 Tanzania
inategemea kuwa na watalii wa matibabu 30,000, mwaka 2040 watalii wa matibabu 68,000 na mwaka 2050 watalii wa matibabu 120,000 watakaotaka kufika Tanzania kupata huduma za
kibingwa na bobezi.
“Kwa mantiki hiyo mwaka 2030 tunauwezo wa kufika dola za
Kimarekani milioni 200, mwaka 2040 tunaweza kupata dola za Kimarekani milioni
420, na mwaka 2050 tunaweza kupata dola za Kimarekani milioni 850”, alisema
Mhe. Balozi Ulanga.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge alisema asilimia 99 ya wagonjwa wa moyo nchini sasa
wanatibiwa ndani ya nchi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 95 zimeokolewa kama
wagonjwa hao wangeenda nje ya nchi.
"Hadi sasa tumefikia mikoa 23 katika programu yetu ya
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services ambapo wananchi wengi wamepata
huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Pia tumefungua matawi ya JKCI
Oysterbay, Kawe, Dar Group, Hospitali ya Chato na kuingia makubaliano na
Hospitali ya Seliani iliyopo Arusha kwaajili ya kuwatibu wagonjwa wa moyo”,
alisema Dkt. Kisenge.


Comments
Post a Comment