Wazazi wahimizwa kuwatibu watoto ugonjwa wa mafindofindo kuwaepusha na magonjwa ya valvu za moyo
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani na mwenzake kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakivuna mshipa wa damu katika mguu wa mgonjwa kwaajili ya kuupandikiza katika moyo wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya upasuaji wa moyo iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Cardiography – ECHO) mgonjwa ambaye mshipa wake mkubwa wa damu (Aorta) umetanuka wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya matibabu hayo iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Maafisa Uuguzi wanaofanya kazi katika chumba cha upasuaji wa
moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Madaktari
Afrika wakiandaa vifaa vya upasuaji wa moyo wakati wa kambi maalumu ya siku nne
iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wataalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi (Heart Lung Machine) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Madaktari Afrika wakijadiliana watakavyosimamisha mzunguko wa damu katika mwili wa mgonjwa wakati upasuaji wa kurekebisha sehemu ya mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ukiendelea wakati wa kambi maalumu ya siku nne iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
********************************************************************************************************
Wazazi wamehimizwa kuwatibu watoto wanaopata ugonjwa wa mafindofindo
(tonsillitis) kuwaepusha na hatari ya kupata magonjwa ya valvu za moyo.
Hayo yamesemwa na Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Salehe Mwinchete wakati wa kambi maaluumu ya siku nne ya
upasuaji wa moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani.
Dkt. Salehe alisema tatizo la valvu za moyo kuziba uanza na
maambukizi ya kooni yajulikanayo kama mafindofindo (tonslight), na homa za utotoni
za mara kwa mara ambazo huleta maambukizi yanayoathiri koo na wadudu wake
kwenda kuharibu milango ya moyo (Valvu za moyo).
Aliongeza kuwa wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wanapougua
mafindofindo ni muhimu wakamuona daktari ili waweze kutibiwa na dawa za
antibiotics kwa usahihi kusaidia kuzuia uharibufu katika milango ya moyo.
“Katika kambi hii iliyomalizika jana tumewafanya uchunguzi
wagonjwa 30 ambapo kati yao wagonjwa 10 tumewafanyia upasuaji wa kuzibua valvu
za moyo kwa kupitia tundu dogo”, alisema Dkt. Salehe
Dkt. Salehe alisema wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa tundu
dogo katika kambi hiyo wana magonjwa ya valvu za moyo ambapo mlango mmoja
katika upande wa kushoto wa moyo unakuwa umeziba au unavujisha damu.
“Dalili za awali za ugonjwa huu ni pamoja na kukosa pumzi,
kuchoka, moyo kwenda mbio, kuzimia mara kwa mara, watu wanapopata dalili hizi
wafike katika Taasisi yetu kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa moyo kwani itawasaidia
kugundua tatizo mapema na kuwaepusha kufikia hatua ya kwenda kufanyiwa upasuaji
wa kufungua kifua”, alisema Dkt. Salehe
Kwa upande wake
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Benjamini alisema wataalamu wa upasuaji wa kufungua
kifua wa JKCI na madaktari Afrika kupitia kambi hiyo wametoa huduma kwa
wagonjwa ambao mishipa yao mikubwa ya damu (Aorta) imetanuka, kupasuka au
imepata vyote viwili kwa pamoja.
Dkt. Alex alisema kupitia kambi hiyo wataalamu waamepata
fursa ya kuongeza ujuzi na kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya
damu kutanuka na kupasuka kutibiwa nchini.
“Matibabu haya ni makubwa na yanahitaji umakini wa hali ya
juu, kupitia kambi hii tumepata fursa ya kujifunza na kuongeza ujuzi”, alisema
Dkt. Alex
Comments
Post a Comment