JKCI kushirikiana na Shirika la Humaniti la Canada kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na huduma za kibinadamu la Humaniti lililopo nchini Canada Firaaz Azeez alipotembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona namna watakavyoshirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na huduma za kibinadamu la Humaniti lililopo nchini Canada walipotembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona namna watakavyoshirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na huduma za kibinadamu la Humaniti lililopo nchini Canada Firaaz Azeez akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona namna watakavyoshirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Shirika hilo Nawal Al-Busaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpa zawadi Nawal Al-Busaidi ambaye ni Mshauri Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na huduma za kibinadamu la Humaniti lililopo nchini Canada alipotembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona namna watakavyoshirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Visiwani Zanzibar.
*************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itashirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na huduma za kibinadamu la Humaniti lililopo nchini Canada katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Visiwani Zanzibar.
Ushirikiano huo utawasaidia watoto wenye matatizo ya moyo
waliopo visiwani humo kupata huduma za matibabu kwa wakati na hivyo kuokoa
maisha yao.
Hayo yamesemwa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akiongea na
viongozi wa Shiriki hilo walipotembelea taasisi hiyo kwaajili ya kuona huduma
za matibabu ya moyo zinazotolewa.
“Ninaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika Taasisi yetu,
kupitia uwekezaji huu hawa wenzetu kutoka nchini Canada wameona waje
kushirikiana na sisi katika kutoa huduma ya matibabu ya moyo kwa watoto waliopo
Zanzibar”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
alisema wataalamu wa JKCI wamekuwa
wakienda Visiwani Zanzibar kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto, kuwepo
kwa ushirikiano huo kutawezesha kupatikana kwa huduma hizo mara kwa mara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa
la Humaniti Firaaz Azeez alisema mwaka 2024 akiwa na wataalamu kutoka Shirika
la Muntada Aid la nchini Uingereza kupitia mradi wa Little Heart walifika katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa
watoto na kujionea vifaa tiba vya kisasa na wataalamu wabobezi waliopo JKCI.
“JKCI ni kituo cha
umahiri cha matibabu ya moyo katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati tumeona
tushirikiane nao katika kutoa huduma za matibabu kibingwa ya moyo kwa watoto waliopo Zanzibar na nchi zingine
za Afrika”.
“Tutashirikiana nao kwa kufanya upimaji, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya waliopo Zanzibar na kutoa uelewa kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo kwa watoto ili watoto wenye matatizo haya waweze kutambuliwa mapema na kupata huduma kwa wakati”, alisema Azeez.
Comments
Post a Comment