Posts

Serikali kufungua tawi la JKCI – Chato

Image
  Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiingia bungeni leo jijini Dodoma kwaajili ya kuwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/25. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakiwa wameshika  hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 kabla haijasoma leo bungeni jijini Dodoma. ************************************************************************************************************************************************************************************** Serikali imepanga kufungua tawi la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Kanda ya Ziwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (JKCI- Chato) iliyopo mkoani Geita. Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/25. Katika kutekeleza hilo Wizara ya Afya moja ya vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha wa 2

Wafundishwa jinsi ya kufanya kipimo cha ECHO

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali namna ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa mafunzo ya wiki mbili kwa wataalamu hao. Jumla ya wataalamu 40 kutoka Hospitali mbalimbali nchini na mmoja kutoka nchini Kenya wanashiriki mafunzo hayo. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Johnstone Kayandabila akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali namna ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa mafunzo ya wiki mbili yanayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wataalamu 40 kutoka Hospitali mbalimbali nchini na mmoja kutoka nchini Kenya wanashiriki mafunzo hayo. Mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Pilly Chillo akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali nchini namna ya kufanya kipim

JKCI yawafuata wagonjwa majumbani

Image

Pata huduma ya matibabu ya moyo kwa njia ya mtandao

Image

Kwa mara ya kwanza upasuaji wa kurekebisha valvu ya moyo wafanyika kwa mtu mzima

Image
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kurekebisha Valvu. ************************************************************************************************************* Kwa mara ya kwanza upasuaji wa kurekebisha valvu za moyo kwa watu wazima umefanyika kwa mgonjwa ambaye valvu yake ya moyo ya upande wa kushoto ilikuwa ikivujisha damu (severe mitral regurgitation). Upasuaji huo umefanywa hivi karibuni na madaktari bingwa wa upasuajia wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka Serikali ya Watu wa China. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Williams Ramadhan alisema upasuaji wa kurekebisha valvu za moyo umekuwa ukifanyika kwa watoto wenye shida za valvu lakini kwa watu wazima mgonjwa huyo amekuwa wa kwanza kurekebishiwa valvu yake kwani wagonjwa wengine wamekuwa wakiwekewa va

Wanafunzi UDSM watoa zawadi kwa watoto wenye matatizo ya moyo na kuchangia damu chupa 14

Image
Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)   mwaka wa Tatu anayesomea    Biashara upande wa Masoko Belinda Mlay akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu ya moyo. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu. Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa Tatu anayesomea Biashara upande wa Masoko Giveness Kitale akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu ya moyo. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu. Mwanachuo wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesomea Biashara upande wa Masoko George Temba akimkabdhi zawadi za watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Msaidizi Grace Sanga. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa: Fanyeni mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwaongaza wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya pamoja aliyoyazindua rasmi leo kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika matembezi ya pamoja yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja aliyoyazindua l