Kampuni ya WATU yatoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 11 kwa JKCI

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea vifaa tiba aina ya Syringe Pump System vyenye thamani ya shilingi milioni 11 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka Kampuni ya Mikopo ya Simu na Vyombo vya Moto (WATU) Patricia Sempinge wakati kampuni hiyo ilipochangia mashine hizo   ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI. 



Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akipokea baadhi ya zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka Kampuni ya Mikopo ya Simu na Vyombo vya Moto (WATU) Patricia Sempinge wakati kampuni hiyo ilivyochangia mashine hizo ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI. 

Mfanyakazi wa Kampuni ya Mikopo ya Simu na Vyombo vya Moto (WATU) akimpatia mzazi wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo zawadi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kutoa vifaa tiba na zawadi kwa watoto katika kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI.

Mfanyakazi wa Kampuni ya Mikopo ya Simu na Vyombo vya Moto (WATU) akimpatia mzazi wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo zawadi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kutoa vifaa tiba na zawadi kwa watoto katika kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka Kampuni ya Mikopo ya Simu na Vyombo vya Moto (WATU) walipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kutoa vifaa tiba aina ya Syringe Pump System vyenye thamani ya shilingi milioni 11 kama sehemu ya kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI. 


Picha na JKCI

*********************************************************************************************

Kampuni ya huduma za mikopo ya simu na vyombo vya moto “Watu” yatoa vifaa tiba aina ya Syringe Pump System vyenye thamani ya shilingi milioni 11 kwaajili ya kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Vifaa hivyo hutumika kuingiza dawa kwa usahihi mkubwa kupitia mishipa ya damu kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo leo katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge aliishukuru kampuni hiyo kwa moyo wa kujitolea na kuona umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya afya.

“Vifaa hivi ni msaada mkubwa kwa wagonjwa wetu na kwa madaktari wanaovitumia katika kutoa huduma lakini pia ushirikiano kama huu una mchango mkubwa katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya moyo nchini”, alisema Dkt. Kisenge

Aidha kupitia mchango huo Dkt. Kisenge amewaomba wadau na makampuni mengine nchini kuiga mfano huo kwa kushirikiana na taasisi za afya kupitia uwajibikaji kwa jamii huku akisisitiza kuwa mchango wa sekta binafsi una nafasi muhimu katika kuimarisha huduma za afya na kuokoa maisha ya wananchi.

“Kampuni ya WATU imekuwa ya mfano kwa kuwafikiria wagonjwa wetu na kutoa vifaa hivi, kampuni nyingine ziendelee kugusa maisha ya wagonjwa wetu na kuwa sehemu ya kuboresha sekta ya afya kwa kushirikiana na Serikali”, alisema Dkt. Kisenge

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja kutoka kampuni ya mikopo ya simu na vyombo vya moto (WATU) Patricia Sempinge alisema kampuni hiyo imeamua kutoa msaada wa mashine hizo na mahitaji mengine ya wagonjwa kwa lengo la kutambua mchango mkubwa unaotolewa na JKCI katika kutoa huduma bingwa na bobezi za magonjwa ya moyo.  

 

“Kampuni ya WATU inaadhimisha miaka mitano ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma za mikopo ya simu pamoja na vyombo vya moto na leo tumefika JKCI kukabidhi mashine hizi ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi hii katika kuokoa maisha ya wagonjwa wa moyo”, alisema Patricia.

Aidha Patricia aliipongeza JKCI kwa kuendesha kampeni ya jua namba zako kwani wamepata fursa ya kupima viashiria muhimu vya afya na kutambua hali zao mapema.

“Magonjwa yasiyoyakuambukiza yanaendelea kuongezeka, hivyo kupata nafasi ya kufanyiwa uchunguzi na kujua namba tano muhimu za afya bila malipo ni fursa muhimu kwetu”, alisema Patricia.



Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma