JKCI yaandika historia yafanya upasuaji wa mshipa mkubwa wa damu (Aorta) kwa kutumia mtambo wa cathlab

Wataalam wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka nchini India Dkt. Gireesh Mukund Warawdekar wakifanya upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab kuziba mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao ulichanika kutokana na ajali raia kutoka Jamhuri ya Watu wa China.

Picha Na

*************************************************************************************************************************

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwezao kutoka nchini India wameandika historia katika kutoa huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu baada ya kufanikiwa kumfanyia upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab mgonjwa ambaye mshipa wake mkubwa wa damu (Aorta) ulichanika kufuatia ajali mbaya ya gari.

Matibabu hayo ya kibingwa ambayo hufanyika katika hospitali chache barani Afrika yamefanyika kwa raia kutoka Jamhuri ya Watu wa China ambaye mara baada ya kupata ajali alipewa rufaa kufika JKCI kwaajili ya matibabu.

Akizungumza kuhusiana na matibabu hayo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa alisema mgonjwa huyo alipata majeraha makubwa baada ya kupata ajali ya gari iliyosababisha kuchanika kwa mshipa mkubwa wa damu (Aorta) unaosafirisha damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Dkt Longopa ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Matibabu ya Moyo alisema mgonjwa huyo baada ya kupata huduma za awali katika hospitali aliyoanzia, madaktari walibaini kuwa mgonjwa alikuwa akipoteza damu nyingi, kupata maumivu makali hivyo kumpa rufaa ili aweze kufanyiwa upasuaji JKCI.

Dkt. Longopa alisema uchunguzi wa kina kwa kutumia mtambo wa CT Scan ulithibitisha kuwa mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ulikuwa umechanika kutokana na nguvu kubwa ya ajali hiyo hali iliyohatarisha maisha yake.

“Baada ya kugundulika kuwa mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ulikuwa umechanika, mgonjwa alihamishiwa JKCI kwaajili ya matibabu ya kibingwa zaidi. Alipofika hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa anaendelea kupoteza damu hivyo ilihitaji uamuzi wa haraka ili kuokoa maisha yake”, alisema Dkt. Longopa

Kwa upande afisa Uuguzi wa chumba cha upasuaji wa kutumia tundu dogo (Cathlab) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna alisema mgonjwa huyo alipokelewa akiwa katika hali mbaya na kupelekwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) kabla ya kupelekwa Cathlab kwaajili ya matibabu.

 “Tunafurahi kuoana upasuaji wa mgonjwa wetu umefanyika vizuri na sasa mgonjwa yupo wodini hali yake imeimarika, madhara yote aliyoyapata baada ya ajali ile tumeweza kuyatatua”, alisema Edna

Mafanikio ya upasuaji huo yanaendelea kuonesha uwezo wa JKCI katika kutoa huduma bingwa na za kisasa kwa wagonjwa wa moyo na mishipa ya damu lakini pia kuimarisha ushirikiano kupitia matibabu kwa wagonjwa kutoka nchi mbalimbali.

-         Mwisho -

Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma