JKCI yaweka kambi ya matibabu ya moyo mkoani Manyara

 

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimsikiliza mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku 5 ya uchunguzi na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH).

Kaimu Mganga Mfawadhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH) Dkt. Yesige Mutajwaa akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kambi maalumu ya siku 5 ya uchunguzi na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH

Wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika kikao cha pamoja na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH) wakati wa kambi maalumu ya siku 5 ya uchunguzi na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.

****************************************************************************************************

Na Picha JKCI

Wananchi wa Mkoa wa Manyara na mikoa ya jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH).

Kambi hiyo maalumu ya siku tano ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inafanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH) iliyopo Mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa kambi hiyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara (MRRH) Dkt. Yasige Mutajwaa aliwaahidi wataalamu wa JKCI kutoa ushirikiano  wa hali ya juu wakati wa kambi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo.

“Wataalamu wetu watashirikiana nanyi ili kwa pamoja tuweze kutekeleza lengo la kuwasogezea huduma bingwa wananchi mahali walipo na kuweza kuwapa elimu kuhusu magonjwa ya moyo kwani magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka katika jamii zetu”, alisema Dkt. Mutajwaa

Kwa upande wake daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo alisema kambi hiyo ni sehemu ya juhudi za kusogeza huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo karibu na wananchi ili waweze kufanyiwa uchunguzi wa mapema na kupata matibabu stahiki lakini pia kupata elimu ya kujikinga na magonjwa ya moyo.

“Hii ni mara yetu ya pili kufanya kambi kama hii mkoani Manyara, mwitikio wa wananchi kushiriki katika kambi hizi kwaajili ya kufanya uchunguzi wa afya umekuwa mkubwa hivyo kutupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma hizi”, alisema Dkt. Pedro

Kambi hiyo itafanyika hadi tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu ambapo wananchi watafanyiwa vipimo vikubwa vya moyo, kuonana na wataalamu mabingwa bobezi wa moyo na wale watakaokutwa na matatizo ya moyo yanayohitaji uchunguzi zaidi kupewa rufaa kufika JKCI kwaajili ya matibabu zaidi.

-      Mwisho - 


Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma