Rais Dkt. Samia aipongeza JKCI kwa kuwafuata wananchi mahali walipo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango iliyofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam. *********************************************************************************************************************************************************************************** Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kutoa huduma ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa kuwafuata wananchi mahali walipo. Pongezi hizo amezitoa jana wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Dkt. Samia alisema taasisi ambazo zinatoa huduma ya kuisaidia jamii kama ambavyo JKCI inafanya zinatakiwa...