JKCI kushirikiana na Misri kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wanamichezo


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Taasisi ya Egyptian African Heart Association iliyopo nchini Misri walipomtembelea ofisini kwake kwaajili ya kujadili namna ambavyo watashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo (Sports Cardiology) jana jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akizungumza wakati viongozi kutoka Taasisi ya Egyptian African Heart Association iliyopo nchini Misri walipomtembelea JKCI kwaajili ya kujadili namna ambavyo watashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo (Sports Cardiology) jana jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Taasisi ya Egyptian African Heart Association iliyopo nchini Misri Ahmed Ashraf Abd Elsalam Eissa akielezea namna taasisi hiyo itakavyoshirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika kutoa huduma za matibabu ya moyo na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanamichezo (Sports Cardiology) nchini walipotembelea JKCI jana jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini