JKCI-ALMC na GSM Foundation wapongezwa kuendesha kambi ya matibabu mkoani Arusha
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre
(JKCI - ALMC) Fabian Bura akimpima shinikizo la damu mkazi wa Arusha aliyefika
katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza
inayofanyika katika Hospitali ya JKCI-ALMC iliyopo jijini Arusha.
Daktari wa macho
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre
(JKCI - ALMC) Wilen Wilson akimpima kipimo cha miwani mkazi wa Arusha aliyefika
katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza
inayofanyika katika Hospitali ya JKCI-ALMC iliyopo jijini Arusha.
Afisa Uhusiano
na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha Lutheran
Medical Centre (JKCI - ALMC) Frida Hellen akiwapatia vipeperushi vinavyotoa
elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza wananchi waliofika katika kambi maalumu ya
uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza inayofanyika katika Hospitali
ya JKCI-ALMC iliyopo jijini Arusha.
Baadhi ya
wananchi wa mkoa wa Arusha wakisuburi kupaa huduma za afya wakati wa kambi
maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza inayofanyika katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre
(JKCI-ALMC) iliyopo jijini Arusha.
Picha na JKCI
*************************************************************************************************************
Wananchi wa mkoa
wa Arusha wameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete – Hospitali ya Arusha
Lutheran Medical Centre (JKCI-ALMC) kwa kushirikiana na Kampuni ya GSM
Foundation kuendesha kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa
yasiyoambukiza mkoani humo.
Pongezi hizo
zimetolewa na wananchi waliojitokeza kufanya uchunguzi wa afya katika kambi
hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete–Hospitali
ya Arusha Lutheran Medical Centre (JKCI–ALMC) iliyopo jijini Arusha.
Wananchi hao walisema
kupitia kambi hiyo wameweza kupata fursa ya kufanya uchunguzi wa afya, kujua
namba zao pamoja na ushauri kutoka kwa watalamu wa afya bila
Aisha Juma mkazi
wa Arusha alisema mbali na wananchi kupata huduma za afya na ushauri kutoka kwa
wataalamu wa JKCI-ALMC wataalamu hao pia wamekuwa wakiwasaidia wanaichi hao
kupata huduma nyingine za jamii kama vile kuwapa viburudisho, kuwasaidia kutoka
sehemu moja kwenda sehemu nyingine wale wasiojiweza na kuchukua mawasiliano yao
kwaajili ya ufuatiliaji wa hali zao.
“Afya ni bora
kuliko pesa, watu wakilijua hili wataona umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya
kuliko kuhangaika na kutafuta pesa kwasababu pesa tunazozitafuta hapo baadaye
zinaweza kutumika hadi kuisha kwa kutafuta huduma za afya”, alisema Aisha
Naye mkazi wa
Arusha mjini John Matemu alisema amefika katika Hospitali hiyo mara baada ya
kupata taarifa hivyo akaona ni muhimu kufika na kufanya uchunguzi wa aya ya
macho yake kutokana na alivyokuwa akijisikia.
“Huduma ni nzuri
na tunazipata kwa wakati, watu wengi wakipata taarifa ya kambi za matibabu
wanahofia muda kutokana na idadi kubwa ya wanaohitaji huduma hizi, lakini hapa
wameweka utaratibu mzuri ambao unarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati”,
alisema John





Comments
Post a Comment