JKCI yafanya upasuaji wa moyo bila kusimamisha moyo kwa wagonjwa watano wenye matatizo ya mishipa ya damu ya moyo kuziba
Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Jaslok iliyopo Mumbai nchini India Upendra Bhalerao wakipandikiza mshipa wa damu kwenye moyo bila kusimamisha moyo (off Pump CABG) kwa mgonjwa aliyefika katika taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano jijini Dar es Salaam.
Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Jaslok iliyopo Mumbai nchini India Upendra Bhalerao wakipandikiza mshipa wa damu kwenye moyo bila kusimamisha moyo (off Pump CABG) kwa mgonjwa aliyefika katika taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano jijini Dar es Salaam.
Picha JKCI
*************************************************************************************************
Na Agnes Sikaonga
Wagonjwa watano wenye matatizo ya mishipa ya damu ya moyo iliyoziba (coronary artery disease) wamefanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu ya moyo bila kusimamisha moyo (off Pump CABG).
Upasuaji
huo umefanyika katika kambi maalumu ya siku tano iliyofanywa na watalaamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka
Hospitali ya Jaslok iliyopo Mumbai nchini India.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kufunga kambi hiyo jijini Dar es Salaam daktari
bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Alex Joseph alisema wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji kwa mafaniko
makubwa.
“Tunawashukuru
hospitali za rufaa kwa kuleta wagonjwa kwani upasuaji umefanyika kwa ufanisi na
wagonjwa wote wanaendelea vizuri na matibabu ambapo wakati wowote tutawaruhusu
kurejea nyumbani”, alisema dkt. Alex
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya
Jaslok iliyopo Mumbai nchini India Upendra Bhalerao alisema watu wenye matatizo
ya mishipa ya damu wanapswa kufika katika taasisi hiyo ili waweze kupatiwa
matibabu mapema.
“Hii
ni mara yangu ya tatu kufanya upasuaji wa namna hii hapa JKCI, na umekuwa
ukifanyika kwa ufanisi mkubwa hivyo niwaombe watu wote ambao mioyo yao
imeshindwa kufanya kazi vizuri kutokana na matatizo ya mishipa ya damu ya moyo
kuziba wafike JKCI ili wapatiwe matibabu ya kisasa”, alisema Dkt. Bhalerao.
Naye
Mkurugenzi wa Taasisi ya Health and Wellness Companion LTD Dkt. Priyank Punatar
alisema Taasisi hiyo imekuwa ikiwaleta
watalaamu kutoka nchini India hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika
kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.
“Namshukuru
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani
amekuwa akisogeza huduma za matibabu ya kibingwa karibu na wananchi wasiokuwa
na uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi”, alisema Punatar.
Ushirikiano
kati ya JKCI na wataalamu kutoka Hospitali ya Jaslok unatajwa kuwa sehemu ya
juhudi za kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa za moyo na mishipa ya
damu nchini pamoja na kuongeza fursa kwa wagonjwa kupata matibabu ndani ya
Tanzania.
-Mwisho-

Comments
Post a Comment