JKCI na NCT wasaini hati ya makubaliona kuimarisha utalii tiba nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge pamoja na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt.
Florian Mtey wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya JKCI na NCT
katika kuhakikisha utalii ndani ya Tanzania unakua salama leo wakati wa hafla
fupi ya kusaini hati iliyofanyika katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuhakikisha
utalii ndani ya Tanzania unakua salama na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii
(NCT) Dkt. Florian Mtey wakati wa hafla fupi ya kusaini hati hiyo iliyofanyika
leo katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge pamoja na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt.
Florian Mtey wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya JKCI na NCT katika
kuhakikisha utalii ndani ya Tanzania unakua salama wakati wa hafla fupi ya
kusaini hati iliyofanyika jana katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es
Salaam.
******************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imesaini hati ya
makubaliano ya ushirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kuimarisha ushirikiano
na kuhakikisha utalii ndani ya Tanzania unakua salama katika eneo la afya na
kuchochea tiba utalili nchini.
Hati hiyo imesainiwa leo jijini Dar es Salaam katika
kutafsiri maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika nyanja ya
afya na utalii kutengeneza mazingira ya kidoplomasia na nchi nyingine duniani.
Akizungumza mara baada ya kusaini hati hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema
kupitia hati hiyo JKCI na NCT watashirikiana kutoa mafunzo kwa waongoza utalii
kwa kuhusisha mafunzo ya awali ya uokoaji wa maisha yatakayowasaidia waongoza
watalii kuokoa maisha ya watalii pale inapotokea changamoto.
Dkt. Kisenge alisema pia watashirikiana katika kuimarisha
huduma kwa mteja hususani katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo
kwa sasa inalenga kukuza utalii tiba kwa kuwatumia vijana wanaochukua kozi za
ukarimu “customer care” kujifunza kwa
vitendo na nadharia katika Taasisi hiyo.
“JKCI na NCT tunaenda kufanya ushirikiano katika kufanya
tafiti na kutoa maandiko yanayohusu utalii tiba nchini ambayo kwa sasa ni
ajenda ya nchi, tafiti hizi zitasaidia kutengeneza mipango endelevu katika
kuchochea tiba utalii nchini”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt.
Florian Mtey alisema lengo la makubaliano kati ya JKCI na NCT ni pamoja na kuendesha
program za kuwafikia watalii na jamii kuhusu msaada wa kiafya.
Dkt. Mtey aliongeza kuwa makubaliano ya ushirikiano huo ni
nyenzo ya kufanikisha na kuimarisha ubora wa huduma katika taasisi hizo mbili.
“Lengo la Serikali ni kufikia watalii milioni 5 na mapato ya
Dola za Marekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025, na eneo hili la watalii
wanaokuja kwaajili ya matibabu ni muhimu pia katika kufikia idadi hiyo”, alisema
Dkt. Mtey
Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na
Chuo cha Taifa cha Utalii ni kielelezo cha dhamira ya pamoja ya kuboresha
huduma na mafunzo katika sekta ya utalii na afya.
Comments
Post a Comment