JKCI yatumia akili mnemba na teknolojia za kidijitali katika matibabu ya moyo
Daktari bingwa wa magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago akizungumza na mkazi wa Singida aliyefika katika banda la taasisi hiyo kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yaliyofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida
.******************************************************************************************************************************************************************************************************************
Na Jeremia Ombelo - Singida
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya teknolojia za kisasa
katika kuboresha huduma za afya kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi
hiyo.
Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa
magonjwa yatokanayo na kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali
ya Dar Group Elias Birago wakati wa Maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
(OSHA) yaliyomalizika leo mkoani Singida.
“Matumizi ya akili mnemba na
teknolojia za kidijitali katika kuimarisha usalama na afya mahali pa kazi,
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imekuwa kinara wa kkwa kuhakikisha tunatangulia
mbele kutumia teknolojia hiyo kwa ufanisi mkubwa”, alisema Dkt. Birago.
Dkt. Birago aliongeza kuwa matumizi ya
teknolojia yamewezesha kupanua wigo wa utoaji huduma na kuweza kuwafikia
wagonjwa walioko mbali na hospitali kwa kutumia tiba mtandao.
“Tumekuwa tukitumia teknolojia ya tiba
mtandao kwa ajili ya kuwafikia wagonjwa wetu ambao wapo nyumbani huku sisi
tukiwa ofisini, wagonjwa wanaotumia teknolojia ya tiba mtandao wanapata huduma
zile zile kama ambavyo wangefika hospitali”, alisema Dkt. Birago
Dkt. Birago amebainisha kuwa mbali na
tiba mtandao, JKCI inafanya uchunguzi wa mwenendo wa shinikizo la damu la
mgonjwa kwa kutumia teknolojia ya kifaa cha DOZEE ambacho kinamwezesha daktari
kufuatilia hali ya mgonjwa akiwa mbali.
“Teknolojia hii ya Dozee inatumika
mgonjwa akiwa nyumbani na daktari akiwa hospitali anaweza kuona taarifa muhimu
za mgonjwa kama mapigo ya moyo na shinikizo la damu (BP) kupitia mfumo huu wa
kidijitali,” alisema Dkt. Birago.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za
kuunga mkono serikali ya awamu ya sita na kuhakikisha teknolojia inatumika kikamilifu katika
utoaji wa huduma za afya hasusani katika magonjwa ya moyo.
Comments
Post a Comment