Viongozi watembelea banda la JKCI maonesho ya Osha

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) na kiwango cha oksijeni mwilini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus aliyetembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuangalia huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wanazozitoa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Dkt. Edith Rwiza akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida.

Picha na: Jeremiah Ombelo

*************************************************************************************************************************


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo