JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa kikao cha wafanyakazi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai akielezea kuhusu maendeleo ya maandalizi kikao
cha CardioTan kinachoandaliwa na Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akijibu hoja za wafanyakazi wakati wa
kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Thadei Kavishe akielezea miundombinu mipya ya maabara inayowekezwa
itakavyopunguza muda wa wagonjwa kusubiria majibu kwa muda mrefu wakati wa
kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akielezea namna kitengo hicho
kimejipanga kuendelea kufanya tafiti mbalimbali wakati wa kikao cha wafanyakazi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupeleka huduma za
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo katika maeneo mbalimbali nchini kwa
kufungua kliniki za matibabu kuwapunguzia wagonjwa adha ya kufuata huduma hizo
Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa kikao na wafanyakazi wa
taasisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa vikao hivyo vinavyofanyika kila baada ya
miezi mitatu.
Dkt. Kisenge alisema JKCI imeanza kufungua kliniki za kutoa
huduma za matibabu ya moyo katika mkoa wa Geita Hospitali ya Chato na mkoani
Arusha kupitia hospitali iliyopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha
(AICC).
“Tumekuwa tukipokea wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali nchini
ambao wanafika JKCI wakiwa wamechoka, kupitia kliniki zetu za Geita na Arusha
wagonjwa waliopo kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa watapata urahisi wa kufika
na kupata huduma kwa wakati”, alisema Dkt. Kisenge
Aidha Dkt. Kisenge alisema JKCI imefanya maboresho ya
miundombinu kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaotibiwa lakini pia
kuifanya hospitali hiyo kuendelea kuwa taasisi bora Afrika Mashariki na Kati.
“Katika maboresho tunayoyafanya tumeweza kuongeza vyumba vya
watu mashuhuli (VIP wards) kutoka vyumba 10 hadi 17 kutokana na uhitaji wa
vyumba hivyo kuwa mkubwa”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Afisa Muuguzi wa JKCI Paulo Josephat
aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi
yanayoongeza motisha wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Paulo alisema maslahi ya wafanyakazi yamekiwezesha Kitengo
cha Utafiti na Mafunzo kuendelea kutoa tafiti bora zinazoielimisha jamii kuhusu
magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo.
“Kitengo cha Utafiti na Mafunzo kinafanya kazi nzuri sana
kupitia tafiti wanazotoa pamoja na kutafuta fedha kutoka kwa wahisani kwaajili
ya wagonjwa wanaotibiwa JKCI wasiokuwa na uwezo wa kulipia matibabu”, alisema
Paulo
Naye Afisa Ubora wa Huduma wa JKCI Hildergard Karau
aliwakumbusha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuvaa vitambulisho wanapokuwa kazini
pamoja na kufuata miongozo ya kazi.
Hilda alisema mfanyakazi anapovaa kitambulisho eneo la kazi kinamsaidia
mgonjwa kuwafahamu watoa huduma wa Taasisi pale mgonjwa anapohitaji kupata
huduma ama maelezo kutoka kwa mtoa huduma.
Comments
Post a Comment