UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO BILA MALIPO TAREHE 28-29/09/2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya moyo duniani itakavyoadhimishwa na taasisi hiyo kwa kufanya matembezi ya hiyari pamoja na kufanya uchunguzi kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja akielezea magonjwa ya moyo kwa
watoto wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya moyo duniani
leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na: JKCI
********************************************************************************************************************************
Katika
kuadhimisha siku ya moyo Duniani tarehe 29/9/2024 Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) tutatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na
matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya
jirani.
Upimaji
huu utafanyika bila malipo yoyote yale kwa watoto na watu wazima tarehe
28-29/09/2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika
kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakata Kikwete (JKCI) iliyopo Kawe jengo la Mkapa
Health Plaza barabara ya Tuari.
Katika
kambi hii kutakuwa na madaktari bingwa wa moyo pamoja na wataalamu wa lishe
watakaotoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na
magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata
ushauri wa kitaalamu.
Pamoja
na upimaji huu tutakuwa na matembezi ya hiyari siku ya jumamosi tarehe 28
Septemba, 2024 yatakayoanzia katika viwanja vya jengo la Palm Village saa 12:00
asubuhi na kumalizikia katika kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakata Kikwete (JKCI)
iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya Tuari.
Matembezi
haya yanafanyika kwa ajili ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kujikinga na
magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.
Tunawaomba
wananchi mjitokeze kwa wingi katika matembezi na kupima afya zenu kujua kama
mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa
mgonjwa.
Kwa
taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754578190, 0783922571 na 0674179036
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.
“Afya ya
Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Imetolewa na:
Dkt. Peter Kisenge - Mkurugenzi Mtendaji
TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Comments
Post a Comment