Wataalamu wa afya watakiwa kutumia lugha rafiki kwa wagonjwa
Mkurugenzi
wa Magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane
akimuelezea Naibu Waziri, ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na wenye Ulemavu
Mhe. Patrobas Paschal Katambi huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo jana katika
Mkutano wa 56 wa Chama Cha Madaktari unaofanyika katika ukumbi wa St. Gasper
Hotel and Conference centre
uliopo jijini Dodoma.
Madaktari
bingwa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa
zikiendelea katika mkutano wa 56 wa chama cha madaktari unaoendelea katika
ukumbi wa St. Gasper Hotel and Conference centre uliopo jijini Dodoma.
***************************************************************************************************************
Madaktari
na wataalamu wa Afya wametakiwa kutumia lugha rafiki kwa wagonjwa kujenga
mahusiano mazuri na kuwapa uhuru kujielezea pale wanapohitaji huduma za
matibabu.
Lugha
rafiki kwa wagonjwa itawasaidia kuelewa na kuwa na uhusiano mzuri na taasisi za
afya hivyo kupelekea ongezeko la jamii kupata elimu na kuwa tayari kupokea
ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.
Akizungumza
jana jijini Dodoma kwenye mkutano wa 56 wa madaktari Naibu Waziri, ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi
alisema jamii inayohitaji huduma za afya haijui maneno ya kisayansi
yanayotumiwa na madaktari hivyo kuwataka madaktari kutumia lugha rafiki ili
jamii iweze kuwaelewa
“Tafuteni lugha rahisi kuwafafanulia wagonjwa
changamoto walizonazo, lakini pia endelezeni uhusiano mzuri baina yenu na watoa
huduma za afya wengine kurahisisha utendaji wenu wa kazi”, alisema Mhe. Katambi
Mhe.
Katambi ambaye alimuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Muhagama katika
mkutano huo alisema siku hizi kesi za wataalamu wa afya kujibu wagonjwa hazipo
bali malalamiko yaliyopo ni kutumia lugha za kitaalamu kuelezea tatizo la
mgonjwa.
Kwa
upande wake mshiriki wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Tatizo Waane alisema ili wananchi waweze kujitokeza na kupata huduma
zinazotolewa katika sekta ya afya muhimu wataalamu wa afya wakawa na uhusiano
mzuri na kujenga uaminifu baina yao.
Aidha Dkt. Waane alisema sera za Serekali
zimeweka umuhimu wa kuchangia huduma za afya ikiwemo huduma za upasuaji wa moyo
hivyo ni muhimu wananchi wakaanza kuchangia huduma za matibabu ya moyo kwani
matibabu hayo ni gharama.
Comments
Post a Comment