Dkt. Kisenge: Jengeni tabia ya kupima magonjwa ya moyo mara kwa m
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wananchi waliofika katika Kliniki mpya ya
JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari wakati wa
kuadhimisha siku ya moyo duniani leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha
siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa
Dar es Salaam bila malipo.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar
es Salaam kupata huduma katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa
Health Plaza Kawe barabara ya Tuari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani
leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa
magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Mkurugenzi wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akielezea tatizo la magonjwa ya moyo lilivyo duniani wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akimpima mtoto kipimo cha kuangalia
jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography –ECHO) wakati wa kuadhimisha siku
ya moyo duniani iliyofanyika katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa
Health Plaza Kawe barabara ya Tuari leo jijini Dar es Salaam. Katika
kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili
kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Christina Yonathan akimpima mtoto kiwango cha oksejeni
mwilini wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika katika kliniki
mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari leo
jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa
magonjwa ya moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sigfrid
Shayo akimsomea majibu mwananchi aliyepatiwa huduma wakati wa kuadhimisha siku
ya moyo duniani iliyofanyika katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa
Health Plaza Kawe barabara ya Tuari leo jijini Dar es Salaam. Katika
kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya moyo wa siku mbili
kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wakisubiri
kupatiwa huduma wakati Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiadhimisha siku
ya moyo duniani kwa kutoa huduma bila malipo kwa wananchi katika kliniki mpya
ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza Kawe barabara ya Tuari leo jijini Dar
es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI imefanya upimaji wa magonjwa ya
moyo wa siku mbili kwa wakazi wa Dar es Salaam bila malipo.
Picha na: Gilbert Mmbaga
*******************************************************************************************************
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipokuwa akizungumza na wananchi
waliojitokeza kupima moyo wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani
iliyofanyika katika kliniki mpya ya JKCI iliyopo Jengo la Mkapa Health Plaza
Kawe barabara ya Tuari jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kisenge alisema duniani zaidi ya watu milioni 20 kwa
mwaka hupoteza maisha ambapo kati yao vifo asilimia 32 hutokana na magonjwa ya
moyo wengi wao wakifariki kutokana na tatizo la mstuko wa moyo.
“Magonjwa ya moyo yanaongezeka kwa kasi kwani hapa nchini
kwetu takwimu zinaonyesha magonjwa haya yanachukua asilimia 13 ya magonjwa yote,
kupitia kauli mbiu yetu ya mwaka huu inayosema “Tumia moyo na chukua hatua ili
kuwasaidia watu wengine kutunza mioyo yao” niwakati sasa jamii ikajilinda ili
iweze kuzilinda familia zao na changamoto ya kumaskini kutokana na gharama za
matibabu”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge aliitaka jamii kubadilisha mtindo wa maisha kwa
kufanya mazoezi, kuacha matumizi ya sigara, kuacha kutumia pombe kwa kiasi
kikubwa, kuzingatia lishe bora na kuepuka vyakula vya wanga na sukari kwa wingi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar
Group Dkt. Tulizo Shemu alisema JKCI
imekuwa mstari wa mbele kuwalinda wananchi kwani kinga ni bora kuliko tiba
hivyo kupeleka huduma za matibabu ya moyo kupelekwa mikoani kupitia kambi maalumu
ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba. Dkt. Shemu alisema mbali na
kupeleka huduma hizo mikoani sasa JKCI imefunga Kliniki Kawe ambayo
imewasogezea huduma karibu wananchi wanaokaa ukanda wa kawe, mbezi chini,
Lugalo, Mwenge, Tegeta na maeneo mengine ya karibu ili wasipate changamoto ya
izifuata huduma hizo Upanga.
“Tumeendelea kuwafikia wananchi kwa kuongeza huduma ili watu
wote wenye mahitaji ya kufika katika taasisi hiyo waweze kupata mbadala wa
karibu na eneo walipo”, alisema Dkt. Shemu
Kwa upande wao wananchi waliopatiwa huduma wakati wa
maadhimisho hayo wameipongeza JKCI kwa kuwa na jitihada za kuisaidia jamii
kuepuka magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo.
Farida Tajiri mkazi wa Mikocheni aliwashukuru wataalamu wa
afya wa JKCI kwa kuwapokea wananchi na kuwapatia huduma kwani hakuwahi kuwaza
kama ipo siku atafanya vipimo vya moyo.
Farida alisema baada ya vipimo amekutwa na shida ya moyo na
kupatiwa dawa, anahisi tatizo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu kwani amekuwa
akijisikia kuchoka na kichwa kuuma sana lakini hakujua kama ni shida ya moyo.
“Nimepokea majibu yangu na kuyakubali, kuanzia leo naenda
kubadilika na kufuata yale niliyoelekezwa na wataalamu hawa pia naenda kuanza
rasmi kliniki ya matibabu ya shinikizo la damu na moyo”, alisema Farida
Naye Juma Mdoe mkazi wa Mbezi Beach alisema baada ya kupata
taarifa ya uchunguzi wa afya unaofanywa na JKCI kutokana na umri wake kuwa
mkubwa aliamua kufika mapema leo na kufanyiwa uchunguzi.
“Sisi wakazi wa maeneo haya tunafurahia kusogezewa huduma
karibu sasa haitatuchukua muda mrefu kuzifuata mjini lakini pia hata tukipata
changamoto usiku mahali pakufika kwa haraka ni hapa”, alisema Juma
Kila ifikapo tarehe 29 septemba dunia uadhimisha siku ya moyo
duniani ambapo JKCI imekuwa ikiadhimisha siku hii kwa kutoa huduma za uchunguzi
na matibabu ya moyo kwa wananchi bila malipo.
Comments
Post a Comment