JKCI na Saudi Arabia kufanya kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Letara na wenzake kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia Omar Almohyzy na Abdulrahman Eisa Redhyan wakijadiliana kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa maandalizi ya kambi maalumu ya siku saba ya upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia Omar Almohyzy na mwenzake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Letara wakiangalia majibu ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mara baada ya kumpima mtoto wakati wa maandalizi ya kambi maalumu ya siku saba ya upasuaji wa moyo kwa watoto 30.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia Omar Almohzy akimfanyia mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa maandalizi ya kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto itakayofanyika kwa siku saba katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kambi hiyo itaanza tarehe 05 Septemba ambapo watoto 30 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo.
***********************************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Kituo cha Mfalme Salman cha
Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia watafanya kambi maalum ya
upasuaji wa moyo kwa watoto.
Kambi
hii itafanyika tarehe 05-14/09/2024 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba wazazi na madaktari wote wenye watoto
wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo hasa wenye matundu ya moyo, matatizo ya
mishipa ya damu na Valve za moyo (ASD, PDA, VSD, TOF & Pulmonary
Valvular Stenosis) wawalete katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata tiba mwafaka.
Aidha tunawaomba wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa. Mgonjwa mmoja anayefanyiwa upasuaji wa moyo anatumia kati ya chupa sita hadi saba za damu. Hivyo basi mahitaji ya damu ni makubwa kwa mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa Moyo.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0715-659333 Dkt. Nuru Letara na 0788-308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Comments
Post a Comment