Kambi maalumu ya matibabu ya magonjwa ya mishipa ya damu iliyotanuka (varicose vain) na ya artert kuziba

 

Wataalamu wa JKCI  wakimzibua mgonjwa mshipa wa damu ulioziba.

***********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalamu wa afya kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu ili watibiwe  katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kuzibua mishipa hiyo.

Matibabu hayo yatakayotolewa tarehe 22 hadi 28 Septemba 2024 yatafanywa na  wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya  Andalusia ya nchini Misri.

Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo ni ya  kuzibua mishipa ya damu ya artery iliyoziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab, upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo katika kutibu mishipa ya damu ya vein iliyotanuka kwa kutumia kifaa cha umeme kijulikanacho kwa jina la laser ablation, kuzibua mishipa ya damu (veins) ya shingo iliyoziba (ballooning) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hasa kwa wagonjwa wa dialysis wanaotumia catheter kwaajili  ya dialysis.

Aidha tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya ganzi miguuni, vidonda vya miguu visivyopona kwa muda mrefu, matatizo ya mishipa ya damu miguuni wafike katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0716-696217 Dkt. Alex Joseph, 0736-110187 Dkt. Tryphone Kagaruki na 0788-308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

"Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu".


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa