Maboresho ya miundombinu yafanyika Hospitali ya JKCI Dar Group
Mhandisi
wa vifaa tiba wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group
Elpidius Prosper akiwaelezea viongozi wa taasisi hiyo maendeleo ya mradi wa
mtambo wa kuzalisha oksijeni wakati viongozi wa taasisi hiyo walipotembelea
miradi mbalimbali ya JKCI leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
akizungumza na daktari wa huduma za dharura Hospitali ya JKCI Dar Group Nicole
Kinyawa wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Taasisi hiyo leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar Group Dkt. Tulizo
Shemu

Mhandisi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucas Paulo akiwaelezea viongozi wa
taasisi hiyo maendeleo ya ukarabati wa chumba cha kufanyia upasuaji wakati
viongozi wa taasisi hiyo walipotembelea miradi mbalimbali ya JKCI leo jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya JKCI Dar Group
wakati wa kikao cha wafanyakazi kujadili maendeleo ya Hospitali kilichofanyika
leo jijini Dar es Salaam.



Picha na: JKCI
************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment