JKCI yapongezwa huduma za kibingwa matibabu ya moyo
Mkurugenzi
wa Magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane
akipokea cheti cha utambuzi wa taasisi hiyo kama mdau wa mkutano wa 56 wa chama
cha madaktari unaoendelea katika ukumbi wa St. Gasper Hotel and Conference
centre uliopo jijini Dodoma.
Daktari
bingwa wa upasuaji wa Moyo na mratibu wa uhakiki na udhibiti ubora wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adelphina Ncheye akitoa maelezo kwa
washiriki wa Mkutano wa 56 wa chama cha
madaktari Tanzania waliotembelea katika banda la JKCI jana jijini Dodoma.
Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kutoka katika mkutano 56 wa Chama Cha Madaktari unaofanyika katika
ukumbi wa St. Gasper Hotel and Conference centre uliopo jijini Dodoma.
Na: Gilbert Mmbaga
*********************************************************************************************************
Naibu Waziri, ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi ameipongeza Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuendelea kutoa huduma za kibingwa bobezi za
matibabu ya moyo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hizo
Aidha
Mhe Katambi ameipongeza taasisi hiyo kwa kuongeza vituo vya utoaji wa huduma za
uchunguzi na matibabu ya moyo katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Pongezi
hizo zimetolewa jana jijini Dodoma alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo
katika Mkutano wa 56 wa chama cha madaktari Tanzania unaofanyika katika ukumbi
wa St. Gasper Hotel and Conference centre.
Mhe.
Katambi ameiomba taasisi hiyo kuendelea kupanua wigo wakutoa huduma za
magtibabu ya moyo na ikiwezekana wafungue matawi ya taasisi hiyo hata nje ya
nchi.
“Nawapongeza
sana JKCI kwa juhudi mnazofanya za kusambaza huduma hizi bobezi za matibabu ya
moyo kwa wagonjwa waliopo nchini na kupunguza furaa za matibabu haya nje ya
nchi”, alisema Mhe. Katambi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo alisema JKCI imekuwa ikitoa mafunzo kwa
wataalamu wa afya katika hospitali mbalimbali nchini kila wanapofanya huduma za
tiba mkoba katika maeneo mbalimbali lengo likiwa kuwajengea uwezo watoa huduma
za afya.
“Kimsingi
nakubaliana na Mhe. Naibu Waziri na kama taasisi tumekuwa kukitoa mafunzo kila
tunapokwenda kutoa huduma za tiba mkoba maeneo mbalimbali nchini”, alisema Dkt.
Pedro
Dkt.
Pedro alisema JKCI imekuwa ikishirikiana na vyuo mbalimbali vya afya ndani na
nje ya nchi kutoa mafunzo kwa wanafunzi ambao ni wataalamu wa afya.
Joseph
Birusha mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma alisema JKCI ikiwa na Chuo
chake itawasaidia wataalamu wa afya ambao wanataka kuchukua fani ya ubingwa
bobezi wa magonjwa ya moyo kuwa na sehemu sahihi zaidi ya kupata masomo hayo.
“Taasisi
za afya za kibingwa zikiwa na vyuo vyake zitawasaidia wataalamu wa afya
wanaotaka kusomea ubingwa bobezi kupata sehemu sahihi ambayo itawawezesha
kusoma na kufanya mazoezi kwa vitendo kuwawezesha kupata ujuzi stahiki”,
alisema Joseph.
Naye
Abdullah Chuma mshiriki wa mkutano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya
Mbeya aliongezea kwa kusema kukiwa na chuo kinachomilikiwa na taasisi ya afya
itasaidia kupata wahudumu wa afya wenye uweledi na umakini kwenye nyanja hiyo.
“Kusoma
kwenye chuo kinachomilikiwa na taasisi inasaidia kupata wahudumu na wataalamu
wa afya waliobobea zaidi, mfano ukisomea JKCI unakuwa mtaalamu wa moyo na
kuweza kuwahudumia wagonjwa wa moyo kwa ufanisi wa hali ya juu kwani ulisoma
sehemu ambayo ulikuwa unaona utoaji huduma unavyofanywa”, alisema Abdullah.
Comments
Post a Comment