Zanzibar waendelea kupata huduma za matibabu ya moyo
Wakazi wa Zanzibar wakiwa katika foleni ya kupata huduma za
uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo wakati wa maonesho
ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport.
Wakazi wa Zanzibar wakipata huduma mbalimbali katika banda la
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya wiki ya Afya
Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akiwafundisha wanafunzi namna huduma za matibabu ya moyo zinavyofanyika wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Heart
Team Africa Foundation (HTAF) Linda Gideon akiwa katika picha ya pamoja na
wakazi wa Zanzibar mara baada ya kuchangia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa
watoto kwa kununua T-shirt wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar
yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar
Picha na: JKCI
*****************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment