JKCI kuwafanyia uchunguzi wa moyo wateja wa ATC
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mashirikiano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Shirika la ndege la Air
Tanzania (ATCL) wakati wa kikao cha kuangalia namna ambavyo watashirikiana
kutoa huduma kwa wateja wanaotumia shirika hilo kupata huduma za uchunguzi wa
afya katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Meneja masoko wa Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL)
Christina Tungalaza akifafanua jambo wakati wa kikao cha kujadili namna shirika
hilo linaenda kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa
huduma za uchunguzi wa afya kwa wateja wake jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akisalimiana na viongozi kutoka Shirika la ndege la Air
Tanzania alipotembelea shirika hilo jana kujadili namna ambavyo watashirikiana
kutoa huduma za uchunguzi wa afya kwa wateja wanaotumia ndege ya ATCL.
Na: JKCI
******************************************************************************************************************
Wateja wanaotumia ndege ya Air Tanzania kupata ofa ya kufanya
uchunguzi wa afya katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Ofa hiyo itatolewa kwa wateja wanaokata tiketi daraja la biashara
(Business) kwa safari za ndani ya nchi na daraja la biashara na uchumi (Business
and Economy) kwa safari za nje ya nchi.
Akizungumza mara baada ya kufanya kikao na viongozi kutoka
shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI imeona fursa ya
kushirikiana na shirika hilo kama sehemu ya kuimarisha tiba utalii nchini.
“Ndege ya Shirika la Air Tanzania sasa inasafiri nchi
mbalimbali Afrika na nje ya Afrika, tukitumia fursa hii kutoa ofa ya uchunguzi
wa afya kwa wateja wake tutakuza utalii tiba nchini”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema JKCI na ATCL wapo katika mkakati wa
kuidhinisha makubaliano ya ushirikiano huo ambao utalifanya Shirika hilo kuwa
la kwanza kuwezesha huduma za uchunguzi wa afya kwa wateja wake nchini.
“Wateja wa Air Tanzania sasa wajiandae kupata huduma bingwa
na bobezi za uchunguzi wa afya katika Taasisi yetu, tunawahaidi mkitibiwa kwetu
hamtaenda hospitali nyingine”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Meneja Masoko kutoka Shirika la ndege la Air
Tanzania (ATCL) Christina Tungalaza alisema ushirikiano na JKCI utasaidia
kuongeza wateja wanaotumia ndege hiyo na kuongeza pato la Taifa.
Christina alisema mbali na kuongeza wateja wanaotumia ndege
hiyo ushirikiano huo utasaidia kupunguza wagonjwa wanaoenda nje ya nchi
kwaajili ya kufanya uchunguzi wa afya kwa kutumia fursa hiyo kuchunguza afya
zao JKCI.
“Tumekuwa tukipata wateja wanaotumia ndege yetu kwenda nje ya
nchi kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu, tukianza ushirikiano na JKCI
itawapunguzia wateja wetu adha ya kufuata huduma za afya nje ya chini na
kutibiwa hapa nchini”, alisema Christina.
Comments
Post a Comment