Mhe. Mazrui aipongeza JKCI kwa kutoa huduma Maonesho ya Afya Zanzibar
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Heart
Team Africa Foundation (HTAF) Linda Gideon akimkabidhi kadi ya kuchangia
matibabu ya moyo kwa watoto mwananchi wa Zanzibar mara baada ya kutoa mchango
wake wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja
vya Hoteli ya Golden Tulip Airport.
Na: JKCI
******************************************************************************************************************
Waziri wa Afya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushiriki maonesho ya wiki ya afya Zanzibar na kutoa elimu ya
namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo pamoja na kutoa huduma za uchunguzi na
matibabu ya magonjwa hayo kwa wakazi wa Zanzibar.
Pongezi hizo zimetolea na Waziri
huyo alipotembelea banda la JKCI lililopo katika maonesho ya Wiki ya Afya
Zanzibar yanayofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport.
“Nawapongeza JKCI kwa kuwafikishia
wakazi wa Zanzibar elimu na huduma hizi muhimu za matibabu ya moyo, mmekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma hizi” alisema
Mhe. Mazrui
Mhe. Mazrui ameitaka JKCI
kuendelea kuwahudumia wakazi wa Zanzibar bila kuchoka kwani wakazi hao
wanawahitaji.
Aidha Mhe. Mazrui ameipongeza
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) kwa kutumia
maonesho hayo kutafuta fedha za kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto
wanaotibiwa JKCI.
Comments
Post a Comment