WACHEZAJI 30 WA TIMU YA TAIFA CHINI YA MIAKA 20 NGORONGORO HEROES WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MOYO
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes wakiwa katika foleni ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wachezaji 30 wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima. Mtaalam wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimtoa damu kapteni wa timu ya taifa chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes Kelvin John kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya mwili wakati wachezaji 30 wa timu hiyo walivyofika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Mauritania mwezi Februari mwaka huu. Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal K...