Wachezaji 29 wa timu ya Taifa Stars wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) wapimwa vipimo vya moyo
Mtaalamu wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimpima kipimo cha damu mchezaji wa timu ya Taifa Stars anayeshiriki mashidano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika (CHAN) Ibrahim Ame Mohamed . Wachezaji 29 wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashidano hayo kupima.
Na Ntiba Nongwe - Dar es Salaam
Wachezaji 29 wa timu ya Taifa Stars wanaocheza ligi za ndani
barani Afrika (CHAN) wamepima vipimo vya
moyo ikiwa ni mojawapo ya
kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki
mashidano hayo apime vipimo hivyo.
Upimaji wa vipimo hivyo
umefanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo wachezaji hao walipimwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography)
umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiograph)
na vipimo vya damu.
Akizungumza na waandishi wa Habari
jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa kurugenzi ya tiba shirikishi Dkt.
Delila Kimambo alisema ni jambo jema kwa
wachezaji hao kupima vipimo vya moyo, kwa kufanya hivyo kutawasaidia
kujua kama wanatatizo au la na kama wanamatatizo
wataweza kuanza tiba mapema na kama
hawana watafuata ushauri wa wataalamu wa afya wa jinsi ya kutunza mioyo yao.
Dkt. Delila ambaye pia ni
daktari bingwa wa magojwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete alisema
mara kwa mara wanawapima wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya mpira ambao wanashiriki
mashidano ya kimataifa jambo linalowafanya wachezaji hao kucheza mpira bila
hofu kwani wanajijua afya zao zikoje.
“Ninawasihi wachezaji
wanaoshiriki michezo mbalimbali kupima afya zao kabla hawajaendelea na mashindano
pia kwa upande wa timu zinazoshiriki ligi mbalimbali hapa nchini zije kupima kwa
kufanya hivyo wachezaji wao wataweza
kushiriki mashindano vizuri “, alisisitiza Dkt. Delila.
Kwa upande wake meneja
wa Taifa Stars Nadir Haroub maarufu kama Canavaro alisema upimaji wa wachezaji hao ni
maelekezo kutoka CAF hivyo basi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linasimamia
upimaji huo ili wachezaji wapimwe na kutambuliwa afya zao.
“CAF wanasisitiza wachezaji wapimwe afya zao ili
wawe na uhakika nao wakiwa na wasisiwasi na majibu ya vipimo vya mchezaji wanarudia
vipimo hivyo. Ndiyo maana kama mnavyowaona wachezaji wetu wamekuja kupima
katika taasisi hii”, alisema Haroub.
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ni Hospitali iliyothibitishwa na CAF kuwa inakidhi vigezo vyote vya upimaji wa
magonjwa ya moyo. Uthibitisho huo ulitolewa kabla ya kuanza kwa mashindano ya
AFCON kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yaliyofanyika mapema mwaka jana hapa nchini . JKCI ilikaguliwa na kuthibitishwa na wakaguzi
kutoka CAF.
Timu mbalimbali
zimeshafanyiwa vipimo hivyo katika Taasisi hiyo zikiwemo Taifa Stars wakati inashiriki
mashidano ya mataifa ya Afrika , Timu ya Simba na timu ya Taifa ya soka la
ufukweni.
Mchezaji wa timu ya Taifa Stars anayeshiriki mashindano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani
barani Afrika (CHAN) Shomari Kapombe akimsikiliza mtaalamu wa
maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay kabla hajampima
kipimo cha damu. Wachezaji 29 wa timu hiyo walifanyiwa
vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo
unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya kutelekeza
sheria ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji
anayeshiriki mashidano hayo kupima vipimo hivyo.
Mchezaji wa timu ya Taifa Stars anayeshiriki
mashidano ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani
barani Afrika (CHAN) Juma Kaseja akisubiri
kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo
unavyofanya kazi na damu na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) . Wachezaji 29 wa timu hiyo wamepima vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya
kutelekeza sheria ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji
anayeshiriki mashidano hayo kupima.
Picha na Gabriel
Johnson - TFF
Comments
Post a Comment