Posts

Showing posts from March, 2026

Kambi Maalum ya Upimaji na Matibabu ya Moyo Yawafikia watu 302 Arusha

Image
Mkurugenzi wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwa sasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watu wazima na Mshauri wa Upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kutoka  National Heart Institute (NHI) nchini Misri Prof. Ghada Kazamel baada ya kumalizika kwa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima iliyokuwa ikifanyika katika Hospitali ya ALMC  na wataalamu wa JKCI, ALMC, Heart to Heart Association for Sustainable Development na  Egyptian African Heart Association (EAHA). Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Goup Eva Wakuganda akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO) mtoto wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanywa na wataalamu wa JKCI, ALMC na   Heart to Heart Association f...

Shilingi milioni 30 zatoa tumaini kwa watoto wenye magonjwa ya Moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea hundi ya Shilingi milioni 30 kutoka kwa viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) walipotembelea Taasisi hiyo jana na kukabidhi mchango huo. Mtendaji Mkuu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt. Naizihijwa Majani akizungumza na viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwashukuru viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  mara baada ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 30 kwaajili ya matibabu ya watot...