Shilingi milioni 30 zatoa tumaini kwa watoto wenye magonjwa ya Moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea hundi ya
Shilingi milioni 30 kutoka kwa viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female
Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
walipotembelea Taasisi hiyo jana na kukabidhi mchango huo.
Mtendaji Mkuu wa
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt.
Naizihijwa Majani akizungumza na viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya
Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwaajili ya kuchangia
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwashukuru viongozi
wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) mara
baada ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 30 kwaajili ya matibabu ya watoto
wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na Taasisi hiyo.
Mtendaji Mkuu wa
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) Dkt.
Naizihijwa Majani akiwaonesha jengo la wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo viongozi
wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) walipotembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jana kwaajili ya kuchangia shilingi milioni 30
kwaajili ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Luciana Myumbilwa akiwaelezea huduma zinazotolewa
katika wodi ya watoto wanaohitaji uangalizi maalumu (PICU) viongozi wanawake
wanaoshiriki mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama
cha Waajiri Tanzania (ATE) walipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya
kuchangia shilingi milioni 30 matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Mbarook akiwaelezea huduma zinazotolewa
katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo viongozi wanawake wanaoshiriki
mafunzo ya Female Future Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) walipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya kuchangia shilingi
milioni 30 matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa
Foundation (HTAF) na viongozi wanawake wanaoshiriki mafunzo ya Female Future
Program msimu 11 yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
walipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya kuchangia shilingi milioni 30
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI.
Na JKCI
****************************************************************************************************
Wanawake wanaoshiriki
mafunzo ya Female Future Program msimu wa 11, yanayotolewa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) wamechangia shilingi milioni 30 kusaidia matibabu ya moyo kwa
watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Fedha hizo zitagharamia
upasuaji wa moyo kwa watoto saba wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo
kiuchumi ambazo hazina uwezo wa kulipia
matibabu, na kurejesha tumaini la maisha bora kwa watoto hao.
Akizungumza wakati wa
hafla fupi ya kupokea mchango huo
iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt.
Peter Kisenge alithamini mchango wa wanawake wa Female Future Program na
kuulinganisha na mchango wa wanawake wa JKCI waliopo mstari wa mbele katika
kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo na kuokoa maisha yao.
"Mmefanya jambo la
kipekee kufika hapa JKCI kuona jinsi wanawake wenzenu wanavyotoa mchango mkubwa
katika kuokoa maisha ya wagonjwa na kushiriki katika shughuli mbalimbali za
kijamii zinazowanufaisha wagonjwa wetu”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema
JKCI inaikomboa Afrika katika masuala ya moyo kwani ni Taasisi pekee inayofanya
kambi maalumu nyingi za uchunguzi na matibabu ya moyo ambazo zimekuwa
zikiwaibua wagonjwa wa moyo katika bara la Africa.
“Bado uhitaji ni mkubwa
ni lazima sisi tujiongeze kuhakikisha tunaisaidia serikali yetu ili kila mtoto
anayezaliwa na changamoto za magonjwa ya moyo asikose huduma”, alisema Dkt.
Kisenge.
Mtendaji Mkuu wa
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) ambayo imekuwa
ikitafuta fedha kutoka kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kulipia gharama za
matibabu ya moyo kwa watoto wasio na uwezo wanaotibiwa JKCI, Dkt. Naizihijwa
Majani alisema matibabu ya moyo ni ya gharama kubwa hivyo inabidi baadhi ya
gharama ziende kwa wananchi lakini kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo wananchi
wengi wanashindwa kuzimudu gharama hizo.
“Baada ya kuanzishwa kwa HTAF stori imekuwa
tofauti kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu kwani
wengi wameweza kunufaika kupitia HTAF. Mwaka 2025 HTAF kupitia hafla ya chakula
cha usiku iliweza kuchangisha shilingi bilioni 2.9 fedha ambazo zimesaidia upasuaji wa moyo kwa watoto 303”.
“Mchango mliotupa ni
mkubwa, mmetoa kwenye mifuko yenu na kuweka katika kikapu kimoja kusaidia
watoto wetu, kwa niaba ya watoto wote watakaonufaika kupitia mchango wenu
tunawashukuru sana”, alisema Dkt. Naizihijwa.
Naye Mwakilishi wa
wanawake washiriki wa Female Future Program, Mhandisi Ester Christopher alisema
wameungana kama wanawake viongozi kuhakikisha wanarejesha tumaini kwa watoto
wenye magonjwa ya moyo, wanafurahi kuona
mchango wao wa shilingi milioni
30 utasaidia upasuaji wa watoto saba.
Mhandisi Ester alisema
wanawake hao ambao ni viongozi kutoka katika Taasisi mbalimblai walipambana na kuungana
kwa pamoja kuhakikisha wanachangia kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya
moyo wanaotibiwa JKCI.
“Tunaupongeza uongozi
wa HTAF kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwa daraja la kuhakikisha watoto
wanapata matibabu lakini pia tunaupongeza uongozi wa JKCI na wataalamu wake kwa
kazi kubwa wanayoifanya ya kuokoa maisha na kurejesha tumaini kwa wagonjwa wa
moyo”, alisema Mhandisi Ester.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama
cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba-Doran alisema viongozi hao hawajamuangusha
kwani wametekeleza kwa vitendo somo la uwajibikaji walilojifunza wakati wa
mafunzo yao.
“Katika kurudisha kwa
jamii viongozi wanawake ambao ni washiriki wa mafunzo ya Female Future Program
msimu 11 wameweza kufika hapa na kutoa mchango wao, tunaomba kwa unyenyekevu
mkubwa mpokee mchango wetu ambao tunaamini utaweza kusaidia na kuokoa maisha”,
alisema Suzanne

Comments
Post a Comment