Afya kwanza! JKCI Dar Group yawafikia watu 527 Kijichi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimjulia hali bibi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizika hivi karibuni Kijichi wilaya ya Temeke na. Zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Steven Kihoko akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizka hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Abderahman Njale akimpima mfumo wa umeme wa moyo mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizka hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Phocus Navath akimsikiliza mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizika hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mkazi wa Mkuranga aliyefika katika kambi maalumu ya uchunguzi wa afya iliyomalizika hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
Wananchi wa Kijichi wakiwa katika foleni ya kupata huduma za uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi wa afya iliyomalizka hivi karibuni Kijichi wilayani Temeke ambapo zaidi ya watu 500 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika kambi hiyo.
******************************************************************************************************************************************************************************************
Watu 527 wamenufaika na huduma za uchunguzi wa afya katika kambi maalumu ya siku tatu iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group kwa wakati wa Kijichi na maeneo jirani wilayani Temeke.
Kambi hiyo ilihusisha vipimo mbalimbali vya
afya vikiwemo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, mfumo wa umeme wa moyo,
shinikizo la damu, kiwango cha sukari
kwenye damu, macho pamoja na uchunguzi wa magonjwa ya kinywa.
Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge
alisema mwitikio wa wananchi umeonyesha haja kubwa ya Taasisi
kuendelea kuwafuata wananchi mahali walipo.
“Katika kambi hii watu 224 tumewapa rufaa ya
kufika katika Hospitali yetu ya Dar Group kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa huduma za upimaji tulizokuwa tunazitoa hapa
kwani tumekutana na changamoto wa wagonjwa wanaoomwa lakini lakini hawaendi
hospitali kupata huduma, za matibabu”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt.
Kisenge ambaye pia ni daktarin bingwa wa magonjwa ya moyo na mtaalamu wa
kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba alisema katika kambi hiyo watu 92
walifanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na watu 118
walifanyiwa kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo.
“Baada
ya kumalizika kwa kambi hii siku ya jumatano tutafanya na kambi nyingine ya
uchunguzi wa afya katika kliniki yetu mpya iliyopo katika Soko Kuu la Kariakoo
ghorofa ya tano, ninawaomba kwa wananchi mje kuchunguza afya zenu kwani huduma
hii itatolewa bila malipo yoyote yale”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Kinywa na
Meno wa JKCI Dar Group alisema kuwa bado
kuna changamoto kubwa kwa wananchi kutozingatia usafi wa kinywa na meno jambo linaweza kusababisha maambukizi
yanayoathiri moyo.
“Moyo unaweza kupata matatizo endapo usafi wa
kinywa na meno hautazingatiwa. Virusi au bakteria kutoka kinywani vinaweza kuingia
kwenye mfumo wa damu na kushambulia moyo”, alisema Dkt. Mvungi.
Aliwahimiza wananchi kusafisha kinywa
mara mbili kwa siku, asubuhi baada ya
kifungua kinywa na usiku baada ya kula chakula ili kuzuia bakteria na virusi vinavyoweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo ya moyo.
Mmoja wa wananchi waliopata huduma katika kambi hiyo Steven Mtambo mkazi wa Mbagala Kizuiani,
aliipongeza JKCI Dar Group kwa kampeni za uchunguzi wa afya zinazowawezesha
watu kutambua hali zao mapema hasa vijana ambao mara nyingi hushughulikia afya
zao pale changamoto za kiafya zinapojitokeza.
Kambi hiyo ya siku tatu, iliyohusisha wakazi wa Kijichi na maeneo jirani ya wilaya ya Temeke, ilizingatia kauli mbiu ya kampeni isemayo “Jua Namba Zako”, inayowaelekeza wananchi kufahamu shinikizo la damu, kiwango cha sukari kwenye damu, urefu, uzito na mafuta mwilini ili kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Comments
Post a Comment