Wanawake zaidi ya 200 wafanyiwa uchunguzi wa saratini ya shingo ya kizazi na matiti

Meneja wa Rasilimali watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Abdulrahman Muya akikabidhi zawadi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.


Mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed akimpatia zawadi mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed akikata keki na Meneja wa Rasilimali watu Hospitali ya Dar Group Abdulrahman Muya na Mwenyekiti wa Chama cha wanawake Dar Group Agnes Mkama wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam

Mtaalamu wa tiba mazoezi (Fiziotherapia) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elizabeth Hyera akimuonesha mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika Hospitali hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed baadhi ya vifaa vinavyotumia kutoa huduma za fiziotherapia wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Frida Felix akimpatia maelekezo mwananchi aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi na matiti wakati wanawake wa Hospitali hiyo walipokuwa wakiadhimisha siku ya wanawake duniani jana jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Beatrice Joseph akimfundisha msichana namna ambavyo saratani inaathiri wakati wanawake wa Hospitali hiyo walipokuwa wakiadhimisha siku ya wanawake duniani jana jijini Dar es Salaam.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mariam Muhenga akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyejitokeza kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani wakati wanawake wa Hospitali hiyo walivyoadhimisha siku ya wanawake duniani jana jijini Dar es Salaam.

Daktari wa magonjwa ya akina mama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mujuni Njunwa akiwafundisha wanawake wa Hospitali hiyo namna ya kukabiliana na moods wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake wa Hospitali hiyo jana jijini Dar es Salaam.


Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao jana jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanywa na wanawake hao jana jijini Dar es Salaam.

Na JKCI
************************************************************************************************

Wanawake zaidi ya 200 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi na matiti na kupatiwa elimu ya namna ya kujilinda dhidi ya magonjwa hayo.

Uchunguzi huo umefanyika jana wakati wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group walipokuwa wakiadhimisha siku ya wanawake duniani katika viwanja vya Hospitali hiyo iliyopo TAZARA jijinin Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho hayo  mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka kutoka Bakhresa Group of Company Mwanafumo Mohamed alisema ni muhimu jamii ikatumia fursa kama hizo zinapojitokeza ili iweze kujifahamu na kuchukua hatua mapema kabla ya kukutwa na changamoto za kiafya.

“Tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kutembelea vituo vya afya na kupima afya zetu mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo kutatusaidia kuyagundua mapema magonjwa haya na kutafuta matibabu mapema”, alisema Mwanafumo

Aidha Mwanafumo aliwapongeza wanawake wa Hospitali hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuchochea maendeleo ya Hospitali kwa kufanya shughuli za kijamii zinazoitambulisha Hospitali kwa wadau mbalimbali.

“Huduma mnazozitoa hapa zimejitosheleza, Tunahitaji kuungana kwa pamoja kuhakikisha tunaikuza Hospitali hii hivyo nawaomba wadau mbalimbali nchini mjitokeze tushirikiane kuongeza upanuzi wa Hospitali hii pamoja na kuwekeza vifaa tiba kwani Hospitali hii inawasaidia wagonjwa wa Temeke, Ilala na wengine kutoka wilaya zote za Dar es Salaam”, alisema Mwanafumo.

Kwa upande wake Meneja Rasilimali Watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Abdulrahman Muya aliwapongeza wanawake wa Hospitali hiyo kwa kujitolea kutoa huduma kwa wanawake wenzao, kutoa elimu itakayoisaidia jamii kubadilika na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa wanaotibiwa na Hospitali hiyo.

Muya alisema wanawake wa Hospitali ya JKCI Dar Group wamewaonesha umuhimu wa kuungana kwa pamoja na kufikia malengo kwani kupitia muunganiko wao waliouanzisha rasmi mwezi septemba mwaka jana wameweza kuadhimisha siku hiyo kwa mafanikio makubwa.

“Huu ni mwanzo mzuri, ni matumaini yangu mtaendelea kuwasogezea huduma wananchi ili waweza kupata fursa ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa haya makubwa yanayoisumbua jamii yetu bila ya kuchoka”, alisema Muya

Naye mwenyekiti wa umoja wa wanawake Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Agnes Mkama alisema mwitikio wa jamii kujitokeza kupima magonjwa ya saratani unaonyesha kuwa wanawake wengi wanatambua umuhimu wa kufatilia afya zao.

Agnes alisema magonjwa ya saratani yamekuwa yakiwakumba wanawake wengi nchini na wengi wao hupata dalili wakiwa katika hatua mbaya jambo ambalo limewafanya wanawake wengi kufika katika Taasisi hiyo kufanyiwa uchunguzi.

“Wanawake wanatakiwa kujitokeza kufanya uchunguzi wa afya hasa katika magonjwa yasiyoambukiza kwani kwa kufanya hivyo watakuwa katika wakati mzuri wa kupata matibabu mapema ama kwa wale ambao hawajapatwa na magonjwa haya watakuwa katika nafasi nzuri ya kujilinda”, alisema Agnes

“Nawahasa wanawake wenzangu kufanya uchunguzi wa saratani angalau kila baada ya miaka mitatu, kwani magonjwa ya saratani yakigundulika mapema kuna uwezekano mkubwa wa kupona kabisa tofauti na yanapogundulika katika hatua za kuchelewa”, alisema Agness

Katika maadhimisho hayo wanawake waliojitokeza wameweza kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa shinikizo la damu, sukari kwenye damu, saratani ya matiti, saratani ya mlango wa kizazi pamoja na ushauri nasaha na msaada wa kiafya.

 

 


 

 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi