Wananchi watakiwa kuiunga mkono Serikali kwa kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa hapa nchini
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akimjulia hali mgonjwa aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia huduma mbalimbali za matibu ya moyo zinazotolewa. Kaimu Mkuu wa Idara ya magonjwa ya moyo kwa watu wazima wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akimuonesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel namna ambavyo mshipa wa damu wa moyo uliokuwa umeziba na kushindwa kupitisha damu vizuri ulivyozibuliwa kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia huduma mbalimbali za matibu ya moyo zinazotolewa. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wat...