WASAMARIA WEMA WAJITOKEZA KUCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WATOTO WAWILI WANAOTIBIWA JKCI
Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa Jamii na Lishe wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Salum akimkabidhi Mr. Jackson
Msilambo Tsh. 4,370,000/= zilizotolewa na Mchungaji Rose Shaboka kutoka kanisa
la New Day Church kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto wake anayetibiwa
JKCI.
Baba wa mtoto anayetibiwa katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Mr. Jackson Msilambo akimpa mkono wa shukrani Mchungaji
Rose Shaboka kutoka kanisa la New Day Church baada ya kukabidhiwa Tsh.
4,370,000 kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto wake anayetibiwa JKCI.
Mchungaji wa kanisa la New Day Church Rose
Shaboka akimjulia hali mtoto wa Jackson Msilambo baada ya kuchangia gharama za
matibabu ya mtoto huyo anayetibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Pia Mchungaji Rose amechangia kiasi cha Tsh.
500,000/= kama gharama za matibabu pamoja na gharama za kupatiwa bima ya afya
kwa mtoto mwingine anayetibiwa JKCI.
Comments
Post a Comment