TAARIFA KWA UMMA
TAHADHARI
KUHUSU WAGONJWA WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU YA MOYO KWA AJILI YA KUTIBIWA
KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Uongozi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) unapenda kuutahadharisha Umma
kuwa waangalifu na wagonjwa wanaochangisha fedha kwa ajili ya kutibiwa
katika Taasisi hii. Ndugu Mwananchi, inawezekana wagonjwa hao wanaochangisha
fedha za matibabu wanakuwa tayari wamepata msamaha wa matibabu kutoka kwa
Taasisi au wasamaria wema wamewalipia.
Kama
utakutana na tangazo la aina hiyo kabla hujamsaidia mhusika tafadhali wasiliana na
uongozi wa Taasisi kupitia namba 0222152392/0782-042010/0688-027982 ili kupata
ufafanuzi.
Imetolewa
na:
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/06/2020
ReplyForward
|
Comments
Post a Comment