Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi azungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito ( Fetal Echoc ardiogram ). Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta watoto wanaotibiwa Jkci kliniki. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza madhara ya mafuta mwilini wagonjwa waliokuwa wanasubiri kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi ( Echocardiogram - ECHO) na Umeme wa moyo ( Electrocardiogram – ECG) wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.