Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yapokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) yenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka kwa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kutoka kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni shilingi milioni 17.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics)  mara baada ya kumkabidhi msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram)  kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni shilingi milioni 17.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics)  kwa msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram)  kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo kwa watoto Dkt. Sulende Khuboja akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha Mafunzo na Utafiti Dkt. Naiz Majani.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari