Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura awa mshindi wa kwanza wa kundi la tafiti za kuzuia magojwa yasiyo ya kuambukiza

Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe akimkabidhi Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura cheti cha mshindi wa kwanza wa kundi la tafiti za kuzuia magojwa yasiyo ya kuambukiza ambaye alifanya utafiti wa kugundua mapema magonjwa ya valvu za moyo kwa watoto wa shule za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam . Dkt. Parvina alikabidhiwa cheti hicho hivi karibuni wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe akimkabidhi Daktari wa Chuo Kikuu cha Dodoma Azan Nyundo cheti cha mshindi wa kwanza wa utafiti alioufanya kuhusu tabia hatarishi za magonnjwa ya moyo kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mirembe wanaotumia dawa za magonjwa ya akili wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililomalizika ...