Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura awa mshindi wa kwanza wa kundi la tafiti za kuzuia magojwa yasiyo ya kuambukiza
Katibu Mkuu wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe akimkabidhi Daktari wa Chuo Kikuu cha Dodoma Azan Nyundo cheti cha mshindi wa kwanza wa utafiti alioufanya kuhusu tabia hatarishi za magonnjwa ya moyo kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mirembe wanaotumia dawa za magonjwa ya akili wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililomalizika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza uzoefu wa taasisi hiyo katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa ya magojwa ya moyo kwa kipindi cha miaka mitano wakati wa kongamano la pili la kitaifa la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililomalizika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam
Salome Majaliwa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya Sekondari waliotembelea banda la Taasisi
hiyo kuhusu huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati wa kongamano la pili la kitaifa
la sayansi la magonjwa yasiyoambukiza lililomalizika hivi karibuni katika ukumbi wa
kimataifa wa mikutano wa mwalimu Julius Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment